Kocha huyo wa kiitaliano tayari ameshaanza na mwanzo mzuri kwa kushinda Germany SuperCup na mchezo wa kwanza wa DFP Cup, lakini malengo makubwa ya klabu yapo katika Bundesliga – “Malengo yetu makuu ni kushinda ligi,” Ancelotti alisema wakati anawasili na kuanza kwa ushindi wa pointi 3 kesho Ijumaa itakuwa ni msingi mzuri kuelekea kutimiza malengo.
Bremen watakuwa wanamtegemea kwa mara nyingine tena mchezaji wa zamani wa Bayern na mmoja wa wafungaji bora wa ligi Claudio Pizarro wakiwa wanajiandaa kuleta mshangao kwa wapenzi wa Bayern.
Takwimu za Mchezo
*Robert Lewandowski alimaliza akiwa mfungaji bora msimu uliopita akiwa na magoli 30.
*Mpaka kufikia leo hii timu hizi zimekutana mara 34 mpaka sasa, katika mechi hizo kila timu imefunga wastani waagoli 3.5 kwa kila mechi. FC Bayern wanaongoza kwa kuwafunga Werder mara 21, sare zipo 6 na Werder nao wameshinda mara 7. Ijumaa hii huu utakuwa mchezo wa kwanza na utaonyeshwa live on Startimes kupitia channel #SportFocus
Majeruhi Upande wa Bayern: Badstuber, Costa, Coman (ankle), Boateng (misuli)
Majeruhi Upande wa Bremen: Garcia, Kruse, Bargfrede
No comments:
Post a Comment