Tuesday, 30 August 2016

Ulinzi waimarishwa Mbarali wakisubiri kupatwa kwa jua

Mbarali. Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune amesema ulinzi na usalama umeimarishwa kwa wageni wa ndani na wale watokao nje ya nchi watakaofika mkoani humo kushuhudia kupatwa kwa jua  Septemba Mosi.

Tukio la kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika eneo la Rujewa, wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Septemba Mosi.

Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake, Mfune amesema  maandalizi yamekamilika ikiwamo utaratibu wa kushuhudia tukio hilo ambalo halijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita.

“Tukio hili ni kubwa na la kihistoria na litawapa fursa ya kuona vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana Mbaralia,” amesema

 Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(Tanapa) Paschal Shelutete amesema tukio hilo litafungua utalii wa ukanda wa kusini.

No comments:

Post a Comment