Friday, 26 August 2016

Tanzania na Ivory Coast Dar kupimana nguvu

Timu ya Taifa ya soka la ufukweni ya Ivory Coast, leo Ijumaa itacheza na Tanzania katika mechi ya kwanza ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu wa ufukweni jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake watakuwa ni Ivan Bayige Kintu pamoja na Muhammad Ssenteza.

Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker kutoka nchini Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo huu wa Dar es Salaam, zitarudiana tena nchini Ivory Coast na mshindi wa jumla ndiye atafuzu kucheza fainali za mashindano hayo.

Kocha wa timu ya Tanzania ni John Mwansasu, mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars na mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja maalumu wa Karume.

No comments:

Post a Comment