Mkurugenzi Masuala ya Katiba na
Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah
Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati
wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali
wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya
haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza
la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi
mbalimbali za Kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki
za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah
Mwaipopo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo
yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya
utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa
kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Masuala ya
Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi.
Nkasori Sarakikya akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi
mbalimbali za Kiraia mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili
mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa
ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa
mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa
matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba
na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi hiyo Bi. Sarah Mwaipopo.
Serikali,kupitia Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya kikao maalumu cha wadau
kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi za kiraia kwa lengo la
kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili ya nchi ya
utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa
kipindi maalum (The Universal Period Review).
Vilevile kikao hicho kitatoa fursa
ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo ya awali kama wadau,
mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa
Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei 2016 , na kuainisha sababu ambazo
zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu
kabla ya kupitishwa rasmi kuwa taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9
Septemba 2016.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi
wa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu
wa Serikali, Bi Sarah Mwaipopo ameeleza kuwa kikao hicho ni hatua
muhimu kkatika mfumo wa maandalizi ya taarifa za usimamizi na
utekelezaji wa haki za binadamu nchini ambao umekua ukishirikisha wadau
wote kutoka Wizara,Idara na Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi zisizo
za kiserikali ambapo amesisitiza wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano
na kutimiza wajibu wao ipasavyo.
“Sote tutambue na kuzingatia
kwamba masuala ya haki za biandamu ni mtambuka na kila mtu ana wajibu wa
kutekeleza na kuyasemea katika eneo lake”alisema Bi Sarah
Halikadhalika,kwa niaba ya
Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekua ikiratibu
kikamilifu maandalizi na uwasilishwaji wa Taarifa zote za masuala
yote ya haki za binadamu kwa kuzingatia mikataba ya Haki za Binadamu
ambayo Tanzania imeridhia na utekelezaji wa jukumu hili umeanishwa
katika Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na
Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Sura ya 268, kifungu cha 14(f) ambayo ni;
kuratibu masuala ya uaandaaji na
utoaji wa taarifa za nchi za utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na
Kimataifa ya haki za binadamu amabyo nchi imeridhia ikiwemo masuala yote
ambayo yanahitaji utolewaji wa taarifa za aina hiyo na kuziwasilisha
kwenye vyombo husika vya Kikanda na Kimataifa kwa ajili ya majadiliano.
Kikao hicho ambacho kitafanyika
kuanzia tarehe 30 -31 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa
na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali,Jukwaa la Katiba Tanzania,Chama cha Watu wenye Ualbino
Tanzania,MISA-TAN,PINGOS’ FORUM,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa,Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania,Uhamiaji,Tume ya
Haki za Binadamu na utawala bora, Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),
Shrikisho la Watu wenye ulemavu Tanzania( SHIVYAWATA) na Msajili wa
Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Kwa upande wa Zanzibar ni Wizara ya
Kilmo na Mifugo, Wizara za Afya,Mifugo, Kazi,Vijana Wazee,Ofisi ya
Mwansheria Mkuu, Jumuia ya Wanawake Wanasheria,Tume ya Uchaguzi
Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi
maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu
ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia
mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania
ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda
na kukuza haki za binadamu nchini mwao.
No comments:
Post a Comment