Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa
Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw.
Sosthenes Sambua na Meneja wa Ofisi wa TECC, Bi. Mwasiti Mkembe (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Mpango Kazi wa miaka
miwili cha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Bi. Beng’i Issa wakati
wa uzinduzi rasmi wa TECC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi.
Beng’i pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bi. Beng’i Issa
(wa pili kulia); mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Hassan Mshinda (katikati) na
Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua (kushoto) wakati wa
uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Bi. Issa pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) wakati Dkt. Mshinda pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Sehemu ya wadau mbalimbali
walioshiriki uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani
Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Habari/Picha Na Ally Daud.
|
Serikali imeahidi kutoa
ushirikiano kuhakikisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania
(TECC) inastawi na kufaidisha wananchi kwa kupitia miradi yake
mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.
Akizungumza hayo katika uzinduzi
rasmi wa TECC Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa
watendelea kuwa pamoja na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya watanzania
kiuchumi.
“Kwa niaba ya serikali natambua
mchango wa wajasiriamali hivyo tupo pamoja na TECC kwa kila jambo
watalofanya kwa ajili ya kusapoti uchumi wa nchi kupitia ujasiriamali
katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mhe. Jenista
Mbali na hayo Mhe. Jenista amesema
kuwa malengo ya TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara
ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya
sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha
biashara zinazoongeza thamani kwa mazao na kutengeneza bidhaa nchini.
Aidha Mhe. Jenista amesema kuwa
Biashara zikianzishwa nyingi na nyingi zikijipanua kiushandi ndivyo na
serikali itapata mapato zaidi kupitia kodi hivyo uzalishaji uongezeke
zaidi na zaidi kwa maendeleo ya nchi.
“Natoa wito kwa taasisi mbalimbali
kuiunga mkono TECC,” alisema, akiongeza kuwa fursa za kusaidia ziko
nyingi kama kuwajengea uwezo kina mama wajasiriamali, wazee wanaostaafu,
au kupanua programu ya Kijana Jiajiri katika mikoa mingine ya Tanzania.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya TECC, Bi. Beng’i Issa alisema tangu kuanza kazi miaka
miwili iliyopita, kwa kutumia rasilimali chache, taasisi hiyo imeweza
kujipanga na kuonyesha mafanikio makubwa katika kujenga uwezo wa
wananchi kumiliki uchumi.
“Tunahitaji kufanya zaidi ya hapa
na uwezo huo tunao kama tutaungwa mkono na Serikali kikamilifu ili
kuweza kutekeleza wajibu wa sera yetu katika kunyanyua wajasiriamali kwa
maendeleo ya taifa,” alisema Bi. Beng’i
Aidha Bi. Beng’i amesema kuwa
mpaka sasa TECC imeshatekeleza miradi miwili muhimu ambayo ni mradi wa
Kijana Jiajiri ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la
Uingereza la Youth Business International (YBI) na kufadhiliwa na umoja
wa makampuni yanayochimba gesi na mafuta katika mikoa ya Mtwara na
Lindi.
Bi. Beng’i amesema kuwa Kupitia
mradi wa Kijana Jiajiri na ufadhili wa shirika la International Youth
Foundation ambalo limepata fedha kutoka Master Card Foundation vijana
1,250 watajengewa uwezo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Pwani na
Dodoma kuanzia mwezi ujao wa Tisa.
Kwa mujibu wa Bi. Beng’i, mradi wa
pili ambao TECC imeufanya ni kwa kushirikiana na mradi wa BEST-Dialogue
wa kufanya utafiti wa maoni ya wamiliki wa biashara ili kupata
changamoto ambazo zinazuia ushindani kibiashara katika mradi wa Business
Leaders Perception.
No comments:
Post a Comment