Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na
wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya
DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali
kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero
wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini
kupatiwa tiba.
kupatiwa tiba.
Huu ni muendelezo wa ziara za
kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na
kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi
wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani
sekta ya Afya.
Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali,
wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.
wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.
Licha ya jengo hilo kujengwa chini
ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla
ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.
Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.
Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu
wa Kituo cha afya Mlali kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya
umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila
Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.
Kwa upande wa wananchi waliofika
kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema
kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa
huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto
kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.
Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie
huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia nakuimarisha Afya
zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana yaHapa Kazi Tu kwa
vitendo.
No comments:
Post a Comment