Madaktari nchini Afrika Kusini wamefanikisha kufanya kwa mafanikio upasuaji wa kuondoa damu iliyoganda kwenye mshipa mdogo wa damu shingoni mwa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.
Kibaki aliripotiwa kuingizwa kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Netcare Sunninghill Jijini Johannesburg, jana asubuhi na kufanyiwa upasuaji kwa muda wa saa moja.
Baada ya kufanyiwa upasuaji huo rais huyo wa zamani Kenya, alirejeshwa wodini na imeelezwa anaendelea vizuri.
Imebanishwa kuwa rais Kibaki atabakia hospitali kwa wiki moja akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.
No comments:
Post a Comment