Thursday, 25 August 2016
Askofu Desmond Tutu amelazwa hospitali mjini Cape Town
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na mwanarakati wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi na utengano nchini Afrika Kusini Askofu Desmond Tutu amelazwa hospitali nchini humo baada ya kuugua maradhi ya kuambukizwa . Kwa mujibu wa binti wa Askofu huyo wa Kanisa la Anglikana, aitwaye Thandeka Tutu, Askofu Tutu, alilazwa katika hospitali moja mjini Cape Town tangu hapo jana na anatarajiwa kuendelea kupata huduma ya matibabu kwa kipindi cha wiki moja au zaidi.
Bado haijafahamika maradhi anayougua Askofu huyo mwenye umri wa miaka 84 ingawa alikuwa akitibiwa pia maradhi ya kuambukizwa wakati alipolazwa tena hospitali mwaka jana. Askofu Tutu ambaye alistaafu harakati za kisiasa na mapambano ya kupigania haki mwaka 2010 siku za nyuma alikuwa akiugua maradhi ya saratani. Tutu alitunukiwa tuzo ya amani mnamo mwaka 1984 kutokana na mapambano yake dhidi ya uliokuwa utawala wa kibaguzi nchini humo.
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment