Matundu ya vyoo katika moja ya shule za msingi nchini
Serikali imewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha
inashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kutatua changamoto ya
ukosefu wa matundu ya vyoo iliyopo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amesema hayo
leo mjini Dodoma katika kikao cha kamati ya utawala na serikali za mitaa
kwa ajili ya kutatua kero ya ukosefu wa madawati na miundombinu mingine
katika sekta ya elimu.Amesema jambo hilo ni la siku nyingi na linatia aibu na serikali peke yake haiwezi kukamilisha mahitaji yote ya matundu yaliyopo hivyo ni vyema wakuu hao wakashirikisha wadau ikiwemo nguvu kazi ya wananchi.
kwa upande wake Mkurugenzi Msimamizi wa Elimu ofisi ya Rais TamisemiJuma Kaponda amesema mahitaji ya matundu ya vyoo upande wa shule za msingi ni 411,517 lakini yaliyopo ni 162,754 na hivyo kuwepo wa upungufu wa matundu 248,763.
Upande wa shule za sekondari mahitaji ni matundu 42,365 wakati matundu yaliyopo ni 23,571 idadi ambayo inafanya uwepo wa upungufu wa matundu 18,784.
Kaponda amesema serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2016/2017 katika mapato ya ndani ya halmashauri imetenga jumla ya shilingi bilioni 10.1 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo 8,791 katika shule za msingi na kwa shule za sekondari imetenga shilingi biliobi 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 1,942.
No comments:
Post a Comment