Thursday, 31 March 2016

Utukufu na Heshima

Hotuba ya Rais Kenyatta Yavurugwa

Wabunge wa Upinzani walipuliza filimbi Bungeni
Hotuba ya Taifa ya Rais wa kenya Uhuru Kenyatta, imetatizwa kwa Muda Bungeni Baada ya Wabuge kadha Wa Upinzani kupuliza filimbi.
Wabunge Hao Walianza kupuliza filimbi na kuvuruga Hotuba ya Rais Punde tu alipoanza kuitoa.



 

Mmoja wa wabunge akizindikizwa nje
Ilimbidi Spika wa Bunge kuwasihi Wabunge ambao walionekana kuendelea kupuliza filimbi.
Hata hivyo Utulivu Ulirejea Baada ya Spika kuwatupa nje wabunge Waliokua wakizipuliza hizo filimbi, na Rais Akaendelea kutoa Hotuba Yake kwa Taifa.

Hodgson Asikitishwa na Wachezaji Wake

 

Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesikitishwa na kikosi chake kukosa Ubunifu Baada Ya kufungwa 2-1 Uholanzi.

Kipigo hicho kimekuja baada ya Uingereza kuonyesha kiwango Bora Wakitoka nyuma na kuwafunga Mabingwa wa dunia Ujerumani mabao 3-2.

Akizungumza baada ya mchezo huo Hodgson amesema pamoja na kumiliki vyema mpira lakini wachezaji Wake Hawakuwa Wabunifu Jambo lilichangia kutotengeneza nafasi za kutosha.

Meneja huyo aliongeza kuwa Hawakucheza vyema kama ilivyokuwa katika Mchezo Dhidi ya Ujerumani kule Berlin.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Uingereza katika Uwanja wa Wembley tangu Novemba Mwaka 2013.

'Walazimishwa Kujenga' Uwanja wa kombe la Dunia Qatar

 

Kundi la Haki za kibinadamu Amnesty International limeishtumu Qatar kwa kuwafanyisha watu kazi kwa lazima katika uwanja utakaochezewa Mechi ya Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022.

Amnesty linasema kuwa wafanyikazi katika uwanja wa Khalifa Wanalazimishwa kuishi katika Mazingira Machafu, Wanalipa fedha Nyingi ili kuajiriwa huku Baadhi ya Mishahara yao ikizuiliwa na kupokonywa Pasipoti zao.



 


  Uwanja wa Kombe la dunia nchini Qatar
Pia imelishtumu Shirikisho la soka Duniani Fifa kwa kushindwa kuzuia Dimba hilo linaloandaliwa Chini ya Unyanyasaji wa haki za kibinadamu.

Qatar imesema kuwa ina wasiwasi kuhusu madai hayo na kwamba itayachunguza.
Serikali ilisema kuwa maslahi ya wafanyikazi wahamiaji yanapewa kipaumbele na kusisitiza kuhusu Marekebisho ya sheria za kazi nchini humo.


 

Uwanja wa kombe la Dunia Qatar
Mwaka uliopita Taifa hilo liliahidi kufanyia Marekebisho Mfumo wa ''Kafala'' ambao Huwazuia Wafanyikazi Wahamiaji kubadilisha kazi ama Hata kuwacha kazi bila idhini ya mwajiri wao.

Lakini Amnesti imeonya kwamba marekebisho hayo Hayataleta Tofauti yoyote na kusema kwamba Baadhi Ya Wafanyakazi ''Wanakabiliwa na wakati mgumu''.

Gary Neville afutwa kazi Valencia

  Neville aliteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa Valencia mwezi Desemba
Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Gary Neville amefutwa kazi Na klabu ya Valencia ya Uhispania Baada ya kuhudumu kama Meneja wao kwa chini ya miezi minne.
Mkufunzi huyo wa Umri wa Miaka 41, ambaye yumo kwenye benchi la kiufundi la Uingereza, alipewa kazi Desemba.

Valencia walishinda mechi tatu pekee kati ya 16 Walizocheza ligi chini ya Neville, na Mechi 10 kati ya 28 kwa Jumla katika mashindano yote

TRA Yakamata Magari Matano ya TFF Kutokana na Malimbikizo ya Kodi ya Bilioni 1.118


Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari Matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.

TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi Mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.

Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo Yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo.

“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama Sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi Ambalo TFF hawajalipa.

“Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia Mwaka 2010 Hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni Billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”

Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.

Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi Ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Wabunge Watatu Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Rushwa

Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
**
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa Mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo

Wabunge hao wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja na kesi itasikilizwa tena April 14

==

Vikundi vya Ujasiliamali Mkuranga Vyashauriwa kuwa katika Mwamvuli wa Vicoba ili Kupata Sifa ya Kukopeshwa

Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa, Bengi Issa mwenye kilemba, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega kushoto kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana naye kuwasaidia na kuwawezesha wananchi wa Mkuranga. Mbunge Mkuranga asaka uwezeshwaji wa wananchi wake

Na Mwamvita Mtanda,  
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, Abdallah Ulega, jana amefanya kikao na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Taifa (NEEC), Bengi Issa, kwa ajili ya kutafuta fursa ya kuwawezesha wananchi wilayani humo.
Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC), Bengi Issa, hayupo pichani.
Kikao hicho pia kilihusisha Mkurugenzi wa Uwezeshaji, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuranga, ambapo Pamoja na mambo mengine, kilijadili namna ya kusaidia vikundi vilivyosajiliwa 285, vikundi vya vicoba 109, ufugaji wa nyuki, vikundi vya wanawake, vijana na waendesha bodaboda.
Akizungumza baada ya kikao hicho kumalizika, Ulega aliyewahi pia kuwa Mkuu wa wilaya Kilwa, Alisema kwamba lengo ni kuona wanananchi wa Mkuranga wanapiga hatua kutoka kwenye hali ya Ukata na kufikia kiwango kizuri, sanjari na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wote.
Alisema kwamba kikao hicho kimemalizika kwa mafanikio ambapo ilishauriwa kuwa vikundi vya kukopeshana (VICOBA) inabidi viwekwe chini ya mwamvuli mmoja utakaoviwakilisha vyote.
“Hili litakapofanyika, Benki ya Posta Tanzania ina utaratibu wa kutoa mikopo ya riba ndogo kupitia Mwamvuli huo unaowakilisha vikundi vyote kwa pamoja, tukiamini kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ndoto zetu.
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunaiweka Mkuranga katika kiwango kizuri ukizingatia kwamba Wilaya hii ipo karibu na jiji la Dar es Salaam, hivyo inaweza kukua kwa kasi kwa sababu mtu anaweza kuishi Mkuranga na akafanya kazi au kuingia na kutoka kwa urahisi wilayani kwetu,” alisema.
Aidha imeshauriwa pia kuanzisha SACCOS ya wafugaji wa nyuki ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo Ya vifaa kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa nyuki, ambapo wana vikundi wanatakiwa kuandaa mpango kazi wao utakaopelekwa Benki ya Maendeleo kwa ajili ya mkopo, ikiwa na lengo la kuhifadhi misitu na kuacha utafutaji wa kipato kwa njia ya kukata miti ili kuzalisha mkaa.

Barabara Ya Kigoma-Nyakanazi Kukamilika Mwezi Mei

1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kigoma tayari kuanza ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika mikoa ya ukanda wa magharibi.
2Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) kuhusu ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na China Railway 50 Group.
3Ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na Kampuni ya  China Railway 50 Group ukiendelea.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa ujenzi wa kampuni ya China Railway 50 Group baada ya kukagua mitambo yao ya kupima na kutafiti udongo kabla ya kujenga barabara.
5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu mara baaada ya kukamatwa kwa vijana wawili (waliokaa chini) kutokana na wizi wa nyaya za mkongo wa taifa, mkoani Kigoma.
6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa koti la kaki) akiangalia athari za mmonyoko wa udongo zilizoathiri mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Kidahwe mkoani Kigoma.
..
Makandarasi wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works.
 
Prof. Mbarawa amewataka makandarasi hao kuongeza kasi ya ujenzi, vifaa na  wafanyakazi wenye sifa ili barabara hizo zikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Tutahakikisha ifikapo Juni mwaka huu tutakuwa tumelipa madeni yote mnayoidai Serikali hivyo fanyeni kazi kwa uhakika kwa kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano tayari tumeshawalipa makandarasi zaidi ya shilingi bilioni 725”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kwamba nia ya Serikali ni kuifungua mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa kwa barabara za lami ili kufungua ukanda wa magharibi mwa nchi kibiashara kutokana na ukanda huo kuwa sehemu muhimu ya nchi katika uzalishaji na kiungo kikuu kwa nchi za Congo DRC, Burundi na Rwanda.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), kulinda miundombinu ya reli na kujiepusha na vitendo vya hujuma ili kuliwezesha shirika hilo kupata shehena kubwa ya mzigo kufuatia wadau mbalimbali kuonesha nia ya kusafirisha mizigo kwa njia ya reli
“Serikali imewekeza vya kutosha katika Shirika la Reli hivyo mfanye kazi kibiashara ili mpate mzigo mkubwa wa kusafirisha”, amesisitiza Prof. Mbarawa
Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma na taasisi zilizo chini ya wizara yake Prof. Mbarawa amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuzuia uvamizi na uhujumu wa miundombinu ya barabara, reli, na mkongo wa taifa wa mawasiliano na wote Watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua za haraka na za kisheria.

Prof. Mbarawa ametoa wiki moja kwa taasisi zilizo chini ya wizara yake kuhakiki wafanyakazi ili kubaini kama kuna wafanyakazi hewa.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa wa Kigoma Umejipanga vizuri katika kudhibiti uvamizi wa miundombinu ya barabara na wale Waliojenga ndani ya mita 22 kwenye barabara kuu wataondolewa maramoja bila kulipwa fidia.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya kanda ya Magharibi ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa uiboreshaji wa miundombinu Ya kanda hiyo ili kuiwezesha kufanya biashara kiurahisi na mikoa mingine ya Tanzania na nchi za Congo DRC, Rwanda na Burundi.

Wednesday, 30 March 2016

Marekani Yalalamikia UN kuhusu Iran


Iran
Image copyright
Marekani na washirika wake kutoka Ulaya wameulalamikia Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ya Iran ya kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Mataifa hayo yamesema majaribio hayo yanakiuka azimio la Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo ambalo liliidhinisha mkataba wa nyuklia baina ya UN na Iran liliitaka Iran kutofanyia majaribio makombora ya masafa marefu yenye uwezo Wa kubeba silaha za nyuklia.
Kwenye barua, iliyopatikana na Reuters, maafisa wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na madai ya Iran kwamba makombora hayo yameungwa mahususi kuwa tishio kwa Israel.
Mataifa hayo manne yameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hatua zinazofaa kuchukuliwa.
Hata hivyo, hayakusema waziwazi kwamba majaribio hayo ya makombora yanakiuka azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Iran.
Makombora hayo yalikuwa yameandikwa kauli mbiu: “Israel sharti iangamizwe”, ikiwa imeandikwa kwa Kiyahudi.

Mkufunzi wa Aston Villa aondoka Baada ya Siku 147


Image copyrightrde
Mkufunzi wa kilabu ya Aston Villa Remi Garde ameondoka katika kilabu hiyo kupitia maelewano baada ya kuhudumu kwa siku 147 katika kilabu hiyo iliopo katika mkia wa jedwali la ligi ya Uingereza.
Remi Garde mwenye umri wa miaka 49 alichukua pahali pake Tim Sherwood katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu ,lakini anaondoka baada ya kushindwa mara sita Mfululizo.
Mechi yake ya mwisho ilikuwa kushindwa kwa 1-0 dhidi ya Swansea mnamo Tarehe 19 mwezi Machi ,matokeo yalioiwacha Villa pointi 12 ikiwa katika hatari ya kushushwa daraja.
Villa ilishinda mechi mbili kati ya 20 wakati wa uongozi wa Garde.
Taarifa ya kilabu ilimshukuru mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kwa juhudi zake wakati wa kipindi kigumu na kusema Erick Black atachukua pahali pake kwa mda.
Uamuzi huo wa kuwachana na Garde unafuatia siku nane za majadiliano Ambayo Yalikamilika siku ya Jumanne.

Millioni 37 Zatengwa Kukarabati Barabara ya kata ya Pazuo/Mkuranga


Na Chrispino Mpinge
JUMLA ya Sh Milioni 37 zimetangwa kwa ajili ya kukarabati
barabara ya Mbogo na Mbezi Muungwana, inayopita katika vijiji kadhaa vya Kata
ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani kwa ajili ya kupunguza adha za ubovu
wa barabara wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo hali inayopelekea wakati
mwingine akina mama kujifungulia njiani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa, Kata ya Panzuo, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.
 
Mapema mwezi uliopita baadhi ya wananchi wakiwamo akina mama
Walizungumza kwa uchungu juu ya ukosefu wa barabara katika maeneo hayo, jambo
linalowanyima raha na ukosefu wa mbinu za kujikwamua kiuchumi kwa kukosekana
barabara inayopitika kwa wakati.
 
Akizungumza juu ya ukosefu wa barabara na mipango yao,
Diwani wa Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, Juma Magaila, alisema
kwamba kiasi hicho cha pesa kitaanzia kwanza kuweka kifusi katika maeneo
Mbalimbali ili wananchi wae ndelee na majukumu yao kwa kuhakikisha kwamba suala
hilo la barabara mbovu linashughulikiwa.
 
Alisema ni kweli wananchi katika maeneo hayo wamekuwa
wakiishi kwa mashaka hususan mvua zinapoanza kunyesha, ila tayari fedha
zimetangwa kwa ajili ya kuanza ukarabati wa barabara hiyo inayotumiwa na
wananchi wengi wilayani Mkuranga.
 
“Tunaendeelea na mikakati ya kuikwamua Kata yetu hususan
katika changamoto kubwa za ubovu wa barabara wanazokutana nazo wananchi wangu
Wa Panzuo ambao wanashindwa kukuza uchumi wao kwasababu barabara haipitiki
kirahisi wakati wote.
 
“Naamini kwa kutengwa kiasi cha Sh Milioni 37 kutachangia
kwa kiasi kikubwa kuiweka barabara yetu katika kiwango cha kupitika huku
Tukielekea katika safari ya kuona tunafikia hatua ya kuiwekea changarawe na
mengineyo,” Alisema.
 
Awali wananchi wa vijiji vya Kibesa wakiongozwa na
Mwenyekiti wao Khamis Ningwe walitumia muda mwingi kuilalamikia barabara hiyo
Sanjari na kuiomba serikali ya Halmashauri ya wilaya Mkuranga iliangalie suala
hilo kwa jicho pevu.
Endapo barabara hiyo itakarabatiwa japo kwa kiwango cha
kifusi, si tu akina mama wajawazito hawatajifungulia njiani kunaponyesha mvua,
Bali wananchi wanaweza kuingiza kipato kwa kuuza bidhaa zao mbalimbali kama
Vile nanasi na nyinginezo zinazopatikana katika maeneo hayo sanjari na kuleta
urahisi watu kuingia na kutoka kwenye maeneo hayo.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU,YAFANYA ZIARA YATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA (JNIA)

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA
 Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza
 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha, akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali (hayupo pichani)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune
 Mjumbe wa Kamati, Anna Richard Lupembe, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, na Mbunge wa Fuoni, Zanzibar, Abbas Ali Hassan Mwinyi, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Ramadhan Maleta, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune (kushoto)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, sehemu ya maegesho ya ndege
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed
Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla,
(kulia kwake) na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Sambali, (wakwanza kulia), sehemu ya maegesho ya ndege
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, ATCL, Johnson Mfinanga akizungumzia hali ya shirika hilo
 Afisa Mkuu wa Masoko wa TAA, Scholastica Mukanjanga, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati, Abass Ali Hassan Mwinyi, (katikati), akizungumza
Sehemu ya jengo la uwanja huo