TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles
Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu,
kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza
kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya
serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani
katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa
19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha kwamba
kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya.
292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa
kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea
taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria
ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi
ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii
kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43
tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi
huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na
kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba
25.
Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa,
Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki
kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na
Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi
ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani)
za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya
mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na
Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.
Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:
No comments:
Post a Comment