Monday, 23 October 2017

Kampuni za simu zimetii sheria ya TCRA

Kampuni sita za simu zilizotozwa faini na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zimetii sheria bila shuruti ndani ya muda uliopangwa.
Julai, TCRA ilizitoza faini kampuni hizo baada ya kushindwa kuzingatia taratibu za usajili wa laini za simu za mkononi. Zilipewa mpaka Oktoba 14 ziwe zimelipa faini hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema licha ya kulipa faini, kampuni hizo zimefanya maboresho ya mtandao katika maeneo yaliyokuwa yanasumbua.
TCRA ilizitoza faini kampuni hizo baada ya kubainika kutumia vitambulisho visivyotambulika na kukiuka taratibu za usajili kwa ujumla.
Kutokana na makosa hayo; Halotel ilitozwa faini ya Sh1.6 bilioni ikifuatiwa na Smart Sh1.3 bilioni na Airtel Sh1.08 bilioni. Nyingine zilikuwa Vodacom Sh945 milioni na Zantel Sh105 milioni.

Kwa kurudia makosa hayo; Halotel ilitozwa Sh822 milioni, Tigo Sh625 milioni na Airtel Sh542 milioni. Zantel Sh52 milioni na Smart Sh37 milioni.

No comments:

Post a Comment