Tuesday 24 October 2017

FFU Ukonga wapigwa marufuku kuwapiga raia

  Image result for sophia mjema
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi cha FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la Ukonga Dar es Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo walichofanya kuwapiga wananchi.
Sophia Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana.
 Mkuu wa Wilaya anasema kuwa askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.
"Kama kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu ulikuwa uchunguzi ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao wangetambulika ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa hiyo nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua wananchi" alisema Mjema


Aidha Mkuu wa Wilaya huyo ametaka wananchi ambao wameumizwa na askari hao kwa vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina ili wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu utafanyika kuona nini kifanyike

No comments:

Post a Comment