Thursday 26 October 2017

Ruto asema alhamisi ya leo ni siku ya furaha kwa wananchi wa Kenya


, Kenya. Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amemaliza kupiga kura na kuielezea siku ya leo Alhamisi ni yenye furaha kubwa kwa vile wananchi wa Kenya watatekeleza moja ya vipengele vilivyomo kwenye katiba ya nchi.
“Nimepiga kura yangu kwa uhuru na amani na siku ya leo ni yenye furaha kubwa kwani wananchi wanashiriki katika uchaguzi kwa amani ili kuipata serikali itakayowaletea maendeleo,” amesema Ruto wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta amepiga kura yake katika kituo cha Shule ya Msingi ya Kosachei eneo la Turbo mjini Eldoret Magharibi mwa Kenya.
  Polisi waingilia kati kulinda amani
Ruto amesema baada ya uchaguzi huo kukamilika wananchi wa Kenya wanapaswa kuanza kushughulika na mambo yanayohusu maendeleo yao na kuicha Serikali itakayochanguliwa kuzitatua kero zao.

“Tumekuwa na kampeni katika kipindi cha mwaka mzima sasa tuanze kutilia mkazo mambo yanayohusu wananchi...wananchi wana changamoto zinazohusu barabara, maji na mambo mengine hivyo macho yetu tuyapeleke huko, “ amesema.

No comments:

Post a Comment