Thursday, 19 October 2017

Kenyatta atangaza maombi kwa Wakenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi itafanya maombi mwisho wa wiki hii kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.
Taarifa ya Rais Kenyatta imekuja baada ya afisa wa cheo cha juu kwenye tume ya uchaguzi nchini Kenya, Kamishna Roselyn Akombe kujiudhulu nafasi yake ndani ya Tume ya uchaguzi ya IEBC mapema leo ambapo katika barua yake ilisema kwamba tume hiyo haina uwezo wa wa kufanya uchaguzi wa haki na huru.
Kenyatta amesema kuwa wakenya watatumia wikendi hii kwa maombi na maridhiano kabla ya uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26 baada ya uchaguzi wa mwezi August kufutwa na mahakama ya juu Septemba Mosi.

Aidha katika uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika wiki ijayo Mpinzani Mkuu wa Rais Kenyatta, Kiongozi Mkuu wa NASA Raila Odinga akiwa amejiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo wa maruduiano.

No comments:

Post a Comment