Tuesday 17 October 2017

Tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'or 2017

Kiungo wa Real Madrid Francisco Román Alarcón Suárez maarufu kama Isco amesema mchezaji pekee anayestahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'or 2017 ni Cristiano Ronaldo.
Akiongea kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya timu yake ya Real Madrid dhidi ya Tottenham Hospur leo, Isco amesema anajisikia faraja kuchaguliwa kwenye orodha ya wachezaji 30 bora wanaowania tuzo hiyo lakini haamini kama anaweza kufikia hatua ya tatu bora.
“Kwangu mimi ni kama ndoto kutajwa kwenye orodha ya wachezaji 30 bora wanaowania tuzo ya Ballon d’or, ni faraja kubwa sana kwangu japo sifikirii kama naweza kufika hatua ya mwisho ya tatu bora, ikitokea hivyo basi itakuwa ni ndoto nyingine”, amesema Isco.
Alipoulizwa kuhusu nani anastahili kutwaa tuzo hiyo, Isco hakupoteza muda alijibu kuwa ni Cristiano Ronaldo. “Ni mchezaji mmoja tu anayestahili tuzo hiyo si mwingine ni Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora na anastahili tuzo hiyo”.

Ronaldo katika msimu uliopita alifanikiwa kutwaa ubingwa wa UEFA pamoja na La Liga kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Real Madrid. Mchezo wa leo kati ya timu hizo mbili utachezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

No comments:

Post a Comment