Monday 30 October 2017

Zidane azidi kuumiza kicha na Barcelona

Kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane amesema bado timu yake ina muda wa kutosha kuweza kupunguza pointi nane ambazo inazidiwa na vinara Barcelona katika LaLiga msimu huu.
Zidane amesema hayo baada ya timu yake kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Girona na kufanya tofauti ya alama kati ya wapinzani hao kuwa nane, Real Madrid ikiwa na alama 20 katika nafasi ya tatu na Barcelona alama 28 kileleni.
Licha ya kupoteza mchezo wa pili msimu huu lakini Zinedine Zidane amesisitiza kuwa mabingwa hao watetezi bado wanaweza kutetea ubingwa wao wa La Liga.
"Najua tunaweza kurejea kwenye ushindi na tukapata pointi na wengine wakapoteza na tukaongoza ligi kwasababu bado muda ni mwingi na mechi bado ni nyingi mpaka msimu ufike mwisho”, amesema Zidane.

Hata hivyo Zidane amegoma kueleza hali ya mlinzi wake Raphael Varane ambaye aliumia kwenye mchezo wa jana ambapo amesema kuwa anasubiri ripoti ya daktari ili kujua endapo atakaa nje ya uwanja au ni maumivu tu ya kawaida na atarejea mapema uwanjani.

No comments:

Post a Comment