Wednesday 25 October 2017

China yatangaza kuachana na mila za urithi

China imetangaza kamati mpya ya viongozi wakuu na kuachana na mila ya kutomtangaza mrithi wa rais Xi Jinping.
Kutotangazwa mrithi kunaashiria kuongezeka ushawishi wa Xi madarakani katika kipindi cha miaka mitano inayokuja, siku moja baada ya jina lake kujumuishwa katika katiba.
Uteuzi huo ulifanywa kwa kamati ya watu inayojulikana kama Politburo, ambayo ina nguvu zaidi nchini China.
Kamati hiyo mpya ilizinduliwa kwenye ukumbi mashuhuri wa watu wa China.
Kando na Xi mwenye umri wa miaka 64, waziri mkuu Li Keqiang, 62, ndiye mwanachama pekee wa kamati ambaye alidumisha nafasi yake.
Viongozi wa China miongo ya hivi karibuni wamekuwa wakimteua mrithi mmoja ua kadhaa katika kamati kuu, wakati wa kuanza kwa muhula wa mwisho kuonyesha warirhi watakaochukua usukani.
kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi anaweeza kuwainua wanachama Chen Miner na Hu Chunhua, wote ambao wana umri wa miaka ya 50 kuweza kuwa warithi wake.
Kamati kuu ya kijehi nayo ilitangazwa. Itaongozwa na Xu Qiliang ambye anadumisha cheo hicho na Zhanga Youxia mshirika waa karibu wa Bw. Xi.
Wajumbe pia waliteua kamati kuu ya nguvu ya wanachama 200 ambao hukutana mara mbili kwa mwaka.
Mashirika ya habari ya kimataifa likiwemo la BBC yalinyimwa vibali vya kuingia ukumbi wa matangazo.

Hatua ya kutoteuliwa kwa warithi wa kamati kuu inampa nguvu zaidi Bw Xi katika miaka mitano inayokuja na kuashiria kuendelea kuwepo kwake baada ya mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment