Tuesday, 10 October 2017

Korea Kaskazini waiba siri za kijeshi za Korea Kusini

Wadukuzi kutoka Korea Kaskazini walidukua mitambo ya kijeshi ya Korea Kusini na kuiba nyaraka nyingi zenye taarifa muhimu za kijeshi.
Miongoni mwa yaliyokuwemo kwenye nyaraka hizo ni mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Mbunge wa Korea Kusini Rhee Cheol-hee amesema taarifa hizo zilitoka kwa wizara ya ulinzi ya Marekani.
Nyaraka hizo zilikuwa na mipango ya karibuni zaidi ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.
Korea Kusini mwezi mei ilifichua kwamba sehemu kubwa ya data iliibiwa na wadukuzi Septemba mwaka jana, madai ambayo Korea Kaskazini ilikanusha.

Jeshi la Korea Kusini limesema kufikia sasa asilimia 80 ya taarifa ambazo ziliibiwa kufuatia udukuzi huo bado hazijatambuliwa.

No comments:

Post a Comment