Rais wa Marekani, Donald Trump ameshtakiwa na watumiaji wa mtandao wa
Twitter aliowafungia wasione anachoandika katika ukurasa wake.
Watu saba wamefungua mashtaka katika mahakama moja jijini New York
nchini humo wakimtaka rais huyo awafungulie kwa kuwa kufanya hivyo ni
kinyume cha Katiba.
Wanasema kwa kuwa Rais wao huwa anatumia ukurasa wake @realDonaldTrump
kutoa taarifa mbalimbali za Serikali, ni haki yao kuona na kujibu
anachoandika.
“Ukurasa wake unawawezesha wananchi kuwasiliana naye moja kwa moja hivyo
ni haki ya kila raia kuweza kuuona, kutufungia ni sawa na kutunyima
haki yetu ya kikatiba ya kupata taarifa,” inasema sehemu ya mashtaka
hayo.
Kabla ya kufungua mashtaka hayo, watu hao waliandika barua kwenda kwa
Rais Trump iliyokuwa na orodha ya majina yao wakitaka awafungulie waweze
kusoma na kujibu anachoandika, hata hivyo, barua hiyo haikujibiwa.
No comments:
Post a Comment