Sunday, 2 July 2017

Upanuzi wa Bandari ya Dar kupaisha uchumi wa Taifa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko amesema upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa maendeleo na ufanisi wa Tanzania ya Viwanda.
Kakoko ameyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi kwa Rais Dk John Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Upanuzi wa Bandari hiyo katika viwanja vya bandari jijini Dar es Salaam.
“Bandari ya Dar es Salaam inahudumia asilimia 90 ya mizigo yote ya ndani na nje. Ina uwezo wa kuhudumia tani milioni 18" Deusdedit Kakoko, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) "Mradi wa uboreshaji wa bandari unatokana na umuhimu wa bandari hii katika kujenga uchumi.
Mradi huu ulianzishwa 2009 baada ya serikali kugundua kuwa bandari hii ingekuwa na uwezo mdogo siku za usoni kama hakutafanywa marekebisho makubwa" Deusdedit Kakoko, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Amesema bandari ya Dar es Salaam Itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena hadi kufikia tani milionj 28 ifikapo mwaka 2028.
Ameongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utapunguza changamoto nyingi tulizonazo kama nchi. Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bella Bird amesema uimara na umadhubuti wa Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi jirani hasa katika ukanda wa maziwa makuu.

"Hii bandari ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na nchi jirani," Bella Bird, Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Amesema mradi unawakilisha mwanzo wa mchakato wa taratibu wa kuinua uwezo wa bandari ya Dar es Salaam na kuimarisha wajibu wake kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

"Nikupongeze wewe na serikali, kwa kuwa jana jiji la Dar es Salaam limetangazwa kuwa mshindi wa 28 wa usafirishaji duniani, na hiyo ni kutokana na mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka. Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza kupata tuzo hii barani Afrika," Bella Bird, Mwakilishi wa Benki ya Dunia

No comments:

Post a Comment