Sunday, 2 July 2017

Tajiri awapa mashabiki wa Chile bendera 5,000 kwaajili ya fainali leo

Mwanabiashara mmoja tajiri nchini Chile ametuma shehena ya bendera elfu tano huko Urusi ambako timu ya taifa lake Chile inapambana na Ujerumani katika mechi ya fainali ya kombe la mashirikisho inayochezwa baadae leo huko St Petersburgs .
Ujerumani ndio mabingwa wa sasa wa kombe la dunia.
Mfanyibiashara huyo wa madini, Leonardo Farkas katika ujumbe wake alioutuma kupitia akaunti yake ya facebook, amewahimiza mashabiki wa Chile nchini Urusi kukusanyika nje ya hotel waliko timu ya Chile, wakati wa saa za chakula cha mchana, ili kuwatakia ushindi na vilevile kupokea viji-bendera hivyo vidogo ambavyo wanavipeperusha wakishabikia na kushangilia.
Mbali na mechi hizi za kombe la shirikisho Urusi itakua pia wenyeji wa kombe la dunia mwaka ujao kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Hii si mara ya kwanza mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 50 ametoa pesa nyingi kuipa motisha timu hiyo ya Chile.

Mwaka 2015 alitoa bendera 40,000 kwa mashabiki waliokuwa wakitazama mechi za Copa America mjini Santiago.

No comments:

Post a Comment