Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi akimkabidhi Mwenyekiti wa halmashauri ya itigi Ally Minja
cheti cha mafunzo ya usimamizi wa miradi ya serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi akizungumza na watumishi, watendaji na madiwani wa
halmashauri ya wilaya ya Itigi (hawapo pichani).
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za Serikali Anna Kakunguru akizungumza katika baraza maalumu la halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi amewataka watumishi kupunguza malalamiko na kuelekeza
nguvu zao katika kuhudumia wananchi kwa mambo yanayoonekana kwa macho.
Dkt Nchimbi ameyasema hayo katika
baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Itigi ambapo amewataka
watumishi na watendaji kupunguza muda wa vikao ili waende kuwatumikia
wananchi.
Amesema kumekuwa na tabia ya
kulalamika ambayo pia inaambukiza kwa watumishi na watendaji wengine
badala ya kutoa suluhisho kwa changamoto ambazo zitawasaidia wananchi.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa
watendaji na madiwani wasitumie muda mwingi ofisini pamoja na kusubiria
taarifa za makaratsi ambazo hazina uhalisia wa matukio na hali halisi
inayoendelea kwa wananchi.
Ameongeza kuwa utendaji wa mazoea
na kulalamika ndiyo husababisha halmashauri kupata hoja za mkaguzi na
mdhibiti wa hesabu za serikali licha ya kuwa na wataalamu wa kutosha
ambao wana vyeti halisi.
Dkt Nchimbi amesema watumishi,
watendaji na madiwani wanapaswa kuzingatia kuwaheshimu, kuwatambua,
kuwathamini na kutowadanganya wananchi katika kuwatumikia kwakuwa
wananchi wana uelewa wa kutosha juu ya mambo mbalimbali.
Aidha katika baraza hilo maalumu,
madiwani wamepokea hoja 37 za mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali
ambapo halmashauri ya itigio imepata hoja 37 na hatiu inayodhirisha.
Dkt Nchimbi amewasisitiza
watumishi, madiwani na viongozi wa halmashauri ya Itigi kufanya kazi kwa
kuzingatia uadilifu na uaminifu ili waweze kuepuka kutengeneza hoja.
Ameongeza kuwa madiwani wasimamie
kwa umakini miradi na shughuli za serikali ili thamani ya fedha iweze
kuonekana kwa miradi hiyo huku akiwashauri kumtumia mkaguzi wa ndani
kama kioo cha kuangalia dosari zao na kuzirekebisha mapema.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Nje wa
Hesabu za Serikali Anna Kakunguru ameishukuru halmashauri ya Itigi
kwa ushirikiano na kuwaasa wasiwe wataalamu wa kujibu hoja bali wawe
wataalamu wa kuzuia hoja.
Kakunguru amesema ofisi ya
Mkaguzi wa nje itaendelea kushirikiana na halmashauri kwakuwa kazi yake
kubwa ni kusimamia sheria zinafuatwa bila kupindishwa.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa
Singida Dkt Angelina M Lutambi amewasa watendaji kuendelea kufuata
maadili ya utumishi wa umma pamoja na maadili na maelekezo wanayopewa
ili kuboresha utendaji wao.
Lutambi ameongeza kuwa kukiuka
maadili na kutowahudumia wananchi ipasavyo ni kitengo cha kurudisha
nyuma jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania za kuwakomboa
wananchi kiuchumi.
Awali katika baraza hilo Mkuu wa
Mkoa wa Singida ametoa vyeti kwa madiwani wa halmashauri ya Itigi baada
ya kuhitimu mafunzo ya kuibua na kusimamia miradi na ruzuku za serikali.
No comments:
Post a Comment