Afisa Sheria Bi. Doris Mugarula
(wakwaza kushoto) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto)
wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea
maendeleo ya biashara yake ya nguo mkoani Arusha.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Bi.
Ghati Muhere (kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi
Hafsa Ali (kushoto) katika duka lake la nguo za kiume, H&D
Collection Shop, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Fedha wa Benki ya KCB Bi.
Happiness Kisanga (wakwanza kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara
mjasiriamali Bi Hawa Mabrouk (katikati) katika ofisi yake ya Video
production, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula
(wakwanza kulia) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa
Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa
Ally (kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani
Morogoro.
Afisa Masoko, wa Benki ya KCB,
Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali
Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani
Morogoro.
Afisa Masoko Bi. Ghati Muhere
(aliyechuchumaa) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa
Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth
(aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Afisa Masoko, Bi. Ghati Muhere
(wakwanza kulia), Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (watatu kushoto) na
Afisa Fedha, Bi Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB
wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Mercy (wakwanza
kushoto) katika biashara yake ya huduma za Interneti mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Bi.
Ghati Muhere (kushoto) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi
Selina (kulia) katika duka lake la bidhaa za watoto Jijini Mwanza.
Afisa Sheria wa Benki ya KCB Bi.
Doris Mugarula (kushoto) akimsikiliza mjasiriamali Bi Fatma (katikati)
akielezea kuhusu biashara yake ya vipodozi na mikoba ya kike Jijini
Mwanza.
Benki ya KCB Tanzania inaendelea
kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya
KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa
2jiajiri. Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko
wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB
2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro
na Zanzibar.
KCB 2jiajiri ni programu
inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo
yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo
yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu
ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua
vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na
kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji,
utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.
“Programu hii ilizinduliwa
rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara
endelevu wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema
Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.
Akielezea kuhusiana na programu
ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri
baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu darasani, kwa sasa wananufaika
kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka kwa washauri watatu
katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.
Akizungumza kuhusiana na mafunzo
ya KCB 2jiajiri, Bi. Janeth Kipangula mjasiliamali mwenye biashara ya
hardware na mfaidika wa KCB 2jiajiri
Aliishukuru Benki ya KCB kwa
kutoa mafunzo ya kibiashara ambayo yamepanua ufahamu wa jinsi
yakuendesha biashara. “kupitia KCB 2jiajiri nimeweza kujua umuhimu wa
kurasimisha biashara, kuwa na leseni ya biashara, kuweka kumbukumbu
katika biashara na jinsi ya kuendesha biashara kiujumla” alisema Bi.
Kipangula.
Benki ya KCB kimsingi inatambua
mchango mkubwa wa wanawake wanaoutoa katika sekta binafsi hususani
katika Ujasiriamali mdogo na wa kati (SMEs) hivyo lengo kwa ujumla ni
kuwezesha wafanyabiashara wanawake wa Kitanzania kuandaa mikakati ambayo
inaboresha stadi zao na uwezo hivyo kuunda fursa nyingi za kibiashara
kwa ajili yao.
Bi. Manyenye alimaliza kwa kusema
kuwa programu ya KCB 2jiajiri ni endelevu na kwa wanawake wajasiriamali
ambao bado hawajajiunga na KCB 2jiajiri wajiulize kwa nini wahangaike
wakati KCB 2jiajiri ipo kwa ajili yao.
No comments:
Post a Comment