Ibada maalum ya Kumuombea Spika Mstaafu Samweli Sita leo imefanyika
jijini dsm leo ikiwa ni siku 40 tangu kufariki dunia nchini Ujerumani
akipatiwa matibabu na kuzikwa mkoani tabora.
Mara baada ya kumalizika ibada hiyo viongozi mbali mbali wa serikali
wakiwemo mawaziri pamoja na manaibu waziri waliopata nafasi ya kutoa
salam wamesema ili kumuenzi marehemu Samweli Sitta hakuna budu kufanya
kazi kwa kujituma,uwazi lakini pia kutanguliza uzalendo na uadilifu.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe amependekeza kuandikwa kitabu ili
kazi alizofanya Marehemu Samweli sitta ziwe katika kumbukumbu,lakini
pia amelishauri bunge la jamhuri kuisimamia vyema serikali ili kumuenzi
marehemu Sitta kwa Vitendo.
No comments:
Post a Comment