Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Marcian Kobello alitoa ufafanuzi
huo kwa wananchi ili kuondoa uvumi ulioenea kuwa noti hiyo, haitatumika
tena kuanzia Desemba 31, mwaka huu.
Alisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli, ni uvumi unaopaswa kupuuzwa na wananchi.
“Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko
sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi itakapotoweka mikononi mwa
wananchi,” alisema.
Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao mbalimbali
ya kijamii kwamba noti hiyo ya Sh 500, haitatumika tena kuanzia Desemba
31, mwaka huu.
Katika siku za karibuni sarafu ya Sh 500 zimekuwa nyingi, tofauti na
zamani, hali inayoashiria kuwa ndio njia ya kuondoa noti hizo mikononi
mwa wananchi.
Pia noti za Sh 500 zimekuwa zikikataliwa mara nyingi na abiria pamoja na
makondakta katika mabasi ya umma, kutokana na mwonekano wake wa
kuchakaa, hali inayosababisha majibizano kati ya abiria na kondakta.
No comments:
Post a Comment