Kinara wa Ligi Luu
Bara, Simba inaondoka leo saa 1:00 asubuhi kwenda Zanzibar kushiriki
Kombe la Mapinduzi ambalo limeanza jana, timu hiyo imetamba kuendeleza
wimbi lake la ushindi kama ilivyo katika Ligi Kuu Bara.
Katika ligi kuu, Simba inaongoza ikiwa na pointi 44 ikifuatiwa na Yanga yenye 40 huku Azam FC ikiwa ya tatu na pointi 30.
Simba ipo Kundi A na
timu za Taifa Jang’ombe, URA, KVZ, Jang’ombe Boys, inatarajiwa kucheza
mechi yake ya kesho Jumapili dhidi ya Taifa Jang’ombe saa 2:30 usiku
kwenye Uwanja wa Amaan, wakitanguliwa na mechi kati ya KVZ na URA saa
10:00 jioni uwanjani hapo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema: “Tunataka kuendeleza kasi yetu ya ushindi kwenye michuano hii ya Mapinduzi, hatutazubaa, tutaifunga kila timu.
“Pia tumepanga kuwatumia wachezaji ambao hatuwatumii sana kwenye ligi ili wapate nafasi ya kuboresha viwango vyao.”
Kati ya wachezaji
ambao hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ni
Laudit Mavugo, Frederick Blagnon, Hamad Juma, Peter Manyika na Novalty
Lufunga.
Mayanja alisema wamepanga kutengeneza mzunguko wa wachezaji katika michuano hiyo na watatoa kipaumbele kwa wachezaji wa benchi.
“Tulichokipanga kama
benchi la ufundi ni kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wetu wa akiba
ambao hawakutumika sana, tunataka kuona uwezo wao wa ndani ya uwanja
baada ya kukosa nafasi ya kucheza.
“Wachezaji hao wa
akiba tutawachanganya na wale wa kikosi cha kwanza tuliokuwa tunawatumia
kwenye ligi kuu na lengo letu ni kuwapumzisha nyota waliotumika sana
katika ligi kuu,” alisema Mayanja.
No comments:
Post a Comment