Na Mwandishi Wetu
Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita anatarajia kuwa mgeni rasmi katika fainali za kuwania Kombe
la Diwani wa Tabata yanayotarajia kuanza Januari nane mwakani kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.
Akizungumza juzi, Diwani wa Kata
ya Tabata, Patrick Assenga alisema ufunguzi wa mashindano hayo mgeni
rasmi anatarajia kuwa Meya wa Ilala Charles Kuyeko.
Assenga alisema kabla ya kuanza
kwa mashindano hayo, Januari 3 anatarajia kukabidhi vifaa vya michezo
kwa timu shiriki 16 vikiwemo jezi na mipira kwa washiriki.
Aseenga alisema mashindano hayo
yatashirikisha timu mbili za mitaa nane ambako mitaa yenyewe ni pamoja
na Tabata, Kisiwani, Msimbazi, Msimbazi Magharibi, Mtambani, Mandela,
Matumbi na Tenge.
Assenga ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Mipango miji wa jiji la Dar es Salaam alitaja zawadi kwa mshindi wa
kwanza ni ng’ombe mkubwa na mpira, mshindi wa pili atazawadiwa ng’ombe
na mpira na mshindi wa tatu atazawadiwa mipira na jezi.
Aidha Assenga alisema katika
ufunguzi wa mashindano hayo atawashirikisha wachezaji wa zamani kama
akina Jella Mtagwa, Peter Tino na wengineo kwa lengo la kuwapa heshima
kwa waliyoifanyia Tanzania miaka iliyopita.
Assenga alisema hamasa hiyo itasaidia wachezaji wa sasa kuongeza hamasa kwa akina Mbwana Samatta ili wasijutie mchezo huo
No comments:
Post a Comment