Beki wa kati wa Yanga, Vincent Bossou
leo Jumatano mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu yake dhidi ya
Ndanda, anatarajia kuchukua mabegi yake na kurejea kwao Togo kwa ajili
ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa hilo ambacho kinajiwinda
kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), ambayo itafanyika nchini
Gabon.
Bossou ni mmoja kati
ya wachezaji watatu watakaokwenda Gabon na timu zao kushiriki Afcon
ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 14. Wengine kutoka
Tanzania ni Juuko Murshid wa Simba na Bruce Kangwa wa Azam.
Bossou ambaye anaunda
ukuta imara wa timu hiyo akisaidiana na Kelvin Yondani, amesema kuwa
anaenda kuungana na wenzake kwa ajili ya kuweka kambi na timu hiyo
ambayo itakuwa Senegal.
“Kesho (leo) baada ya
mechi na Ndanda naondoka na kurejea nyumbani kuungana na wenzangu
kwenye timu ya taifa kuweka kambi ndogo kwa ajili ya kujiandaa kushiriki
Afcon ambapo sisi ni moja ya timu shiriki.
“Baada ya kufika
huko tunaenda Senegal ambapo ndipo kutakuwa na kambi rasmi na
nitakosekana katika Kombe la Mapinduzi kwa sababu nipo huku lakini
naamini kila kitu kitakuwa sawa kwani kuna watu wengi wanaoweza kucheza
nafasi yangu,” alisema Bossou.
No comments:
Post a Comment