Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa nne
kulia mbele) akiwasili wilayani Karatu kwa ajili ya kuwapatia hati
miliki za Ardhi jamii ya wa Hadzabe.
Wa Hadzabe wakimkaribisha Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kwa kumvusha taji.
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akiwapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi
wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Wa Hadzabe wakifurahi na Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Lukuvi baada ya kuwapa hati miliki za Ardhi.
Wakazi wa kijiji cha Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha
wakisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi,
ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua.
Wakazi wa kijiji cha Mang’ola juu wilayani Karatu Mkoani Arusha
waliosimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi wakimsikiliza wakati akitatua
mgogoro wao wa Ardhi.
Na Kitengo cha Mawasiliano – Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewapatia hati miliki za Ardhi
kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri Lukuvi amefika katika
maeneo yao na kuwapa hati miliki za kimila kwa vijiji na wanayoishi
jamii ya wa Hadzabe na jamii nyingine za kifugaji ili kulinda maeneo yao
ya malisho na maeneo wanayotumia kuwinda wanyama.
Jamii ya wa Hadzabe ni watu ambao
huishi kwa mfumo wa maisha ya kuwinda, kufuga wanyama pori na kula mimea
na matunda ya miti inayowazunguka. Jamii hii kwa miaka mingi imekuwa
ikiishi bila kufuata mipaka ya maeneo yao na hivyo kusababisha migogoro
ya ardhi kwa jamii nyingine zinazoishi karibu na maeneo yao.
Pamoja na ziara hiyo Mhe. William
Lukuvi amtatua migogoro ya Ardhi ya wananchi wa wilayani Karatu Mkoani
Arusha na wananchi walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzipatia
ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi
walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.
Wananchi wa vijiji vya Mang’ola
juu na Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha walisimamisha msafara wa
Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi
alisimama na kuzitatua pamoja na kumuagiza Mkuu wa wilaya ya karatu Bibi
Therezia Mahongo kutafutia ufumbuzi baadhi ya migogoro hiyo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za
utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika
kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na
ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya
mwezi huu wa Desemba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na
wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa
Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa
Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.
Pia Mhe. Lukuvi ametatua migogoro
ya ardhi ya Mkoa wa Mara katika wilaya za Musoma na Bunda ambapo kwa
Arusha ametatua migogoro ya wilaya ya Arumeru na Karatu.
No comments:
Post a Comment