PAUL Kagame, Rais wa Rwanda amesema hana mpango wakujiunga na Mahakama
ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa madai ya kuundwa kisiasa,
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuhitimisha Baraza la Taifa
la Umushirikiano (NUC) amesema, ICC imekuwa ikishiriki katika kuihujumu
Afrika.
Na kwamba, mahakama hiyo imeshindwa kuangazia viongozi wa mataifa ya Magharibi huku ikiwalenga zaidi Waafrika pekee.
Amedai, Rwanda inapopozungumzia jambo lolote kuhusu mahakama hiyo,
imekuwa ikilazimishwa kukaa kimya kwa madai inashawishi matifa mengine
ya Afrika kuungana nayo.
“Rwanda haiwezi kujiunga na ICC kwa kuwa chombo hicho sio cha haki,
kiliundwa kisiasa kama chombo cha haki cha kimataifa lakini utendaji
wake ni wa mamashaka…” amesema na kuongeza;
“Rwanda ikilizungumzia hili, tunaambiwa tusizungumzie lolote juu ya ICC
kwasababu tunaonekana kuchochea mataifa mengine. Kimsingi tunapaswa
kujifunza kwamba, ni lazima tuwe huru na kujitegemea.”
Hata hivyo, amepinga kitendo cha baadhi ya watu kushirikiana na mataifa
ya kigeni kukosoa mataifa yao kwa maslahi binafsi “mimi napingana na
kutetea hulka ya mataifa mengine kwa maslahi binafsi.”
Mwaka 2013 Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa tifa hilo
aliikosoa mahakama hiyo kwamba ni ya kisiasa “Rwanda haiwezi kuiamini
mahakama hiyo kamwe,”alinukuliwa Mushikiwabo.
Rwanda haikujiunga ICC hali inayofanya taifa hilo kutumia upenyo huo
kuikosoa vikali hususan wakati huu ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika
yanatangaza kuikacha.
No comments:
Post a Comment