Sunday, 25 December 2016

Moyes: Nilitaka kuwasajili Bale, Kroos na Fabregas Man United

Utamaduni mkubwa katika klabu ya Manchester United umepotea kulingana na aliyekuwa mkufunzi wa klabu hiyo ambaye sasa ndio meneja wa Sunderland David Moyes.
Raia huyo wa Uskochi alipigwa kalamu na United 2014 baada ya kuchaguliwa kumrithi meneja Alex Ferguson.

Amesema kuwa klabu hiyo ililenga kuwateua wakufunzi wa Uingereza na kwamba haikuwa na mpango wa kujiweka katika soko la uhamisho.
''Ninaweza kusema hayo yote yamekwisha.Kumekuwa na mabdiliko kiasi katika klabu ya Manchester United lakini hivyo ndivyo walivyoamua kuelekea''.

United imetumia pauni milioni 480 tangu Ferguson astaafu 2013 baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 26.

"Wakati nilipomlenga kumleta Gareth Bale nilihisi tangu kitambo kwamba Bale ni mchezaji wa Manchester United.Nilipigana hadi dakika ya mwisho .Tulitoa kitita kikubwa ikilinganishwa na Real Madrid ,lakini Bale tayari alikuwa ashaamua kwenda Real Madrid.Huyo ndiye mchezaji niliyetaka kumleta Manchester United. Mchezaji mwengine alikuwa Cesc Fabregas, ambaye tulidhani tutamsajili hadi dakika za mwisho.

Nakumbuka wakati nilipokutana na Sir Alex na nikadhani kwamba kulikuwa na fursa kubwa ya kumleta Ronaldo.
"Kwa hivyo hicho ndicho kilichokuwa kiwango tulichokuwa tukilenga. Sikuwa na lengo la kuwanuanu wachezaji saba au nane kwa sababu tulikuwa na kikosi ambacho kilikuwa kimeshinda ligi''.
Toni Kross alikuwa amekubali kuja United. Tulikuwa tumekubaliana na Toni mwenyewe pamoja na ajenti wake. Mara nyengine mipango haiendi vile na unavyotaka. Tulitaka kumsajili Bale .Usajili wa Cesc ndio uliotuvunja moyo.Tulikuwa karibu sana. Na Toni Kroos alikuja January tukidhani tumefunga kazi.

No comments:

Post a Comment