Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewasimamisha kazi watumishi
watano akiwemo aliekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Liwale, Gaudence Nyamihura na Aliekuwa mganga mkuu wa wilaya hiyo
Daktari Martin Mwandike ambae kwa sasa amehamishiwa Wilayani Rufiji Ili
kupisha uchunguzi wa upotevu wa vifaa tiba vya upasuaji katika kituo cha
afya cha Kibutuka vilivyopotea mwaka 2013.
Akiwa katika siku yake ya pili ya ziara yake wilayani Liwale, Mkuu wa
mkoa wa Lindi Godfrey Zambi pamoja na kukagua shughuli za maendeleo
wilayani humo alipata fursa ya kuhutubia mikutano mbalimbali ya hadhara
ambapo katika mkutano uliofanyika kata ya kibutuka alipokea kero ya
upotevu wa vifaa hivyo.
Kufuatia Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwake katika taarifa ya kata hiyo
pamoja na wananchi,Zambi alitoa Agizo la kusimamishwa kazi kwa
waliohusika na ambao walishindwa kuwajibika kwa nafasi zao Utumishi.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya kibutuka, Dkt Odoroth
Ndimbo ambae alipewa fursa kuelezea upotevu huo katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya kata hiyo alikuwa na
haya kusema.
Watumishi waliotangazwa kusimamishwa kazi ni pamoja na Aliekuwa
mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Gaudence Nyamihura ambae kwa sasa yupo
ofisi ya katibu tawala mkoa wa Lindi, Aliekuwa mganga mkuu wa wilaya,
Dkt Martin Mwandike ambae kwa sasa amehamishiwa wilaya ya Kibiti.
Wengine ni Aliekuwa Afisa Utumishi wakati tukio lilipotokea mwaka 2013
ambae sasa amehamishiwa wilaya ya Newala, Bw Mfaume Kassim pamoja na
Mfamansia msaidizi wa wilaya, Mohamed Nyagali.
No comments:
Post a Comment