Azam FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.
Uamuzi wa Azam umekuja baada ya
mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu
tangu ‘wahispaniola’ walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya
Stewart Hall kubwaga manyanga.
“Uongozi wa Azam FC umewatimua
makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja
mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili,”
chanzo cha kuaminika toka ndani ya Azam FC .
Katika mechi 17 za VPL ambazo
Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda
mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne
(4).
No comments:
Post a Comment