Na.Alex Mathias.
Baada ya African Lyon
kuibeba Simba wekundu wa Msimbazi hao watashuka dimbani kucheza na timu
ya JKT Ruvu Stars kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Simba bado wanaongoza
Ligi wakiwa na pointi 38 huku watani zao Yanga baada ya kukabwa koo na
Lyon bado wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 37 na kama Simba
atashinda mchezo huo atakuwa ameongeza gape la pointi nne na kuendelea
kukalia usukani.
Hata hivyo Simba
itawakosa washambuliaji wake hatari Ibrahimu Ajibu aliyekwenda nchini
Misri kufanya majaribio ya kucheza soka la kimataifa pamoja na Frederick
Blagnon ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi
ya Ndanda FC ambapo waliibuka na ushindi wa magoli 2-0.
Kwa Upande wa
matajiri wa jiji la Dar es salaam,Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina
tofauti ya pointi 12 na vinara Simba katika Ligi Kuu Bara, sasa
imejigamba leo ni lazima iwafunge Majimaji ugenini ili kupunguza
utofauti wa pointi hizo.
Azam ina pointi 26
katika mechi 16 ilizocheza ambapo kati ya hizo, imeshinda mechi saba,
imefungwa mara nne na imetoka sare mara tano, imefunga mabao 21 na
imefungwa mabao 14.
Mchezo wa Azam na
Majimaji unachezwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma
na Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amesema: “Lazima tushinde.”
Timu hizo zinakutana
katika Uwanja wa Majimaji leo ambapo Azam ina historia ya kutofungwa
katika uwanja huo na wapinzani wao hao.
Akizungumza, Idd
alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na ametamba
wataendeleza ushindi wao kwa wapinzani wao hao ili wachukue pointi tatu
muhimu.
“Kocha ameyafanyia
marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mechi yetu na African Lyon na
tuna imani tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa kesho (leo) ili kuweza
kuendeleza rekodi yetu kwani hatujafungwa na Majimaji katika uwanja
wao.
“Kikosi kipo vizuri
na wachezaji wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo isipokuwa tutawakosa
wachezaji watatu ambao ni Daniel Amoah, Mudathir Yahaya na Gadiel
Michael ambao ni majeruhi,” alisema Idd.
Kwa upande wake Kocha
wa Majimaji, Kali Ongalla, alisema: “Mechi hii ni ngumu, wenzetu wana
wachezaji wengi wa kigeni, ila tutapambana ili tushinde.”
Michezo mengine:Mbeya
City vs Toto African,Kagera Sugar vs Stand United,Mwadui FC vs Mbao
FC,Ndanda FC vs Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons.
No comments:
Post a Comment