. Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Tanzania, imelipa Sh 687 milioni za kodi ya pango iliyokuwa inadaiwa na Manispaa ya Kinondoni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema fedha hizo ni malipo ya kuanzia mwaka 2009 hadi 2016 ya pango ya ofisi za kampuni hiyo.
Amesema wametekeleza agizo hilo kabla ya siku saba walizopewa kulipa na fedha hizo zote zinaelekezwa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa ya kwenda sekondari anakwenda.
“Wanafunzi wasiopungua 3,000 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2017/18 hawajapata nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
“Wilaya ya Kinondoni ina uhaba wa vyumba 79, kwa fedha hizi tutajenga vyumba 40 hivyo kupunguza tatizo kwa kiasi kikubwa”, alisema Hapi.
No comments:
Post a Comment