Jina la Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ndani ya
msikiti uliopo kwenye Kijiji cha Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa
Kaskazini Pemba kumesabisha vurugu.
Waumini wa walikubaliana kutotaja kabisa jina la Dk. Shein kwenye
msikiti huo kutokana na makovu ya kisiasa yaliyotokea kwenye Uchaguzi
Mkuu uliopita lakini mtoa mawaidha wa msikiti huo kwenye swala ya Ijumaa
iliyopita alitaja jina hilo.
Mzozo ulianza baada ya jina la Dk. Shein kutajwa ndani ya msikiti huo
huku waumini wakionesha kukerwa kwa mtoa mawaida huyo, taratibu mzozo
ukaanza kuibuka.
Hata hivyo, kabla ya vurugu kuwa kuwa, baadhi ya waumini kutokana na
kukerwa na jina la Dk. Shein ndani ya msikiti huo, waliamua kutoka nje.
Ilipofika usiku wa saa tatu, Jeshi la Polisi lilivamia msikiti huo uliogomea kutajwa jina la Dk. Shein na kuanza kupiga mabomu.
Mtoa taarifa anasema, baada ya polisi kuvamia na kupiga mabomu, hali ya
taharuki ilitanda na kusababisha watu wanaoishi jirani na msikiti huo
kuanza kukimbia.
Kuzuka kwa vurugu hizo msikitini kunathibitishwa na Haji Khamisi Haji,
Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambaye alisema, aliwatuma vijana wake usiku
kwa ajili ya kutuliza hali ya sintofahamu kwenye msikiti huo.
Amesema kuwa, hatua hiyo ilitokana na baadhi ya waumini wa kutaka
kuuchoma moto msikiti huo kutokana na mgogoro huo. Hata hivyo alieleza
kutokuwa na taarifa za polisi kupigwa mabomu.
Ndani ya msikiti huo kumegawika pande mbili; mmoja unaunga mkono
kutajwa jina la Dk. Shein huku lingine likipiga marufuku jina hilo.
Said Ahmad Muhammad, Ofisa wa Ofisi ya Mufti wa Taasisi ya Kiislam
anayeshughulikia Fatwa (maamuzi) amesema, kuwa mgogoro kwenye msikiti
huo anaujua.
Na kwamba, pande hizo zilieleza umuhimu wa kutuingiza masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada.
Hata hivyo, baada ya pande hizo mbili kuelezwa umuhimu wa kutenganisha
siasa na ibada, walikubaliana kuwa Dk. Shein hatotajwa tena kwenye
msikiti huo na kuwa, ameshangaa jina hilo kutajwa kinyume na
makubaliano.
No comments:
Post a Comment