Tuesday, 2 August 2016

Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Mwanza

RPC MSANGIMNAMO TAREHE 31.07.2016 MAJIRA YA SAA 5:10 ASUBUHI KATIKA MAENEO YA ILEMELA MLIMANI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU AMBAO NI 1.BONIPHACE MASAMAKI MIAKA 47, 2. LINA COSMAS MIAKA 26 NA 3. ALI MOHAMED MIAKA 30 WOTE WAKAZI WA MTAA WA ILEMELA MLIMANI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIUNGANISHIA UMEME KINYEMELA KWENYE NYUMBA ZAO KINYUME NA SHERIA NA UTARATIBU ULIOWEKWA NA TANESCO.

AIDHA WATUHUMIWA HAO WALIWEZA KUKAMATWA BAADA YA KUPATIKANA KWA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA, NDIPO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAOFISA WA TANESCO WALIWEZA KUFANYA MSAKO MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU.
WATUHUMIWA WOTE WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA TANESCO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. MSAKO WA KUWASAKA WATU WENGINE AMBAO WAMEJIUNGANISHIA UMEME KINYUME NA UTARATIBU BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKAO WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIWEKEA UMEME KINYEMELA KATIKA NYUMBA ZAO KWANI NI KOSA LA JINAI LAKINI PIA WANAHATARISHA MAISHA YA FAMILIA PAMOJA NA MALI ZAO, HIVYO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WEMA NA MAOFISA
WA TANESCO LITAHAKIKISHA LINAWASAKA NA KUWATIA NGUVUNI WATU WOTE WANAODAIWA KUJIWEKEA UMEME KINYEMELA KWENYE NYUMBA ZAO NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 30.07.2016 MAJIRA YA SAA 4:30 ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA BUKINI KIJIJI CHA CHIFULE KATA YA BUKUNGU TARAFA YA UKARA WILAYA YA UKEREWE MKOANI MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA ZEPHANIA BITA MIAKA 42 MFANYABIASHARA NA MKAZI WA KITONGOJI CHA BUKUMIA ALIFARIKI DUNIA KWA AJALI YA MOTO ULIOWAKA WAKATI WAKIMIMINA MAFUTA AINA YA PETROL NA MWENZAKE ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA DOTTO AMBAE AMEJERUHIWA KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA NDANI YA NYUMBA YAKE CHUMBANI NA MWENZAKE TAJWA HAPO JUU, HIVYO WAKATI WANAMIMINA MAFUTA HAYO YA PETROL KWENYE MADUMU ALIPITA MTU KWENYE KORIDO YA NYUMBA HIYO AKIWA ANAVUTA SIGARA NA KUPELEKEA KUZUKA KWA MOTO ULIOMUUNGUZA MAREHEMU MWILI MZIMA NA KUSABABISHA MAJERAHA BWANA DOTTO AMBAYE HALI YAKE BADO AIDHA MOTO HUO UMESABABISHA MADHARA MENGINE YA KUUNGUA KWA VYUMBA VINNE PAMOJA NA KUTEKETEA KWA MALI ZILIZOKUWEPO NDANI YA NYUMBA HIYO,THAMANI HALISI YA VITU NA MALI ZILIZOTEKETEA KATIKA AJILI HIYO BADO HAIJAFAHAMIKA, MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE KWA MATIBABU LAKINI HALI YAKE BADO SIO NZURI. JESHI LA POLISI BADO LIPO KATIKA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA AJALI HIYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUJIHADHARI WAKATI WOTE PINDI WANAPOFANYA KAZI ZA HATARI ILI KUWEZA KUZUIA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA, LAKINI PIA AMEWATAKA WATU WENYE TABIA YA KUFANYABIASHARA ZA MAFUTA YA PETROL NA DIESEL ZISIZO HALALI KISHERIA KUACHA MARA MOJA.
IMETOLEWA NA
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Post a Comment