Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Rukwa
Arch. Deocles Alphonce wakati alipokagua ujenzi wa ofisi za Bonde la
Ziwa Rukwa na Maabara zake zilizopo Sumbawanga Mjini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua
nondo zilizosukwa kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kalambo lililopo
katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112,
Mkoani Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na
ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu
wa KM 112, Mkoani Rukwa.
Mhandisi
Mshauri wa Kampuni ya Nicholas O’Dwyer Eng. Farley Vicente akitoa
taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa kuhusu ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye
urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa China Railway 15 Bureau Group Corporation
kutoka China Zhang Tonggang (mwenye sweta nyekundu) inayojenga barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112 kwa kiwango cha lami,
Mkoani Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihakiki
taarifa za mapato katika Bandari ya Kasanga iliyopo Mkoani Rukwa.
Katikati ni Msimamizi wa bandari hiyo Bw. Seleman Kalugendo.
Meneja
wa Shirika la Posta Tanzania Bi. Zahara Sukeiman akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu
huduma ya kutuma na kupokea Vifurushi wakati Waziri alipotembelea
ofisini hapo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
Maelekezo kwa Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) nyanda za juu
kusini Bw. Peter Kaguru wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoani Rukwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kupunguza idadi ya vikao vya
baraza visivyo na ulazima ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha na
badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye uendelezaji wa miundombinu ya
bandari za maziwa.
Ametoa agizo hilo mara baada ya
kukagua shughuli za utendaji wa bandari ya Kasanga iliyopo mkoani Rukwa
inayohudumia mkoa wa Kigoma, nchi ya Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo (DRC) ambapo amebaini mapungufu ya kiutendaji ikiwemo malipo
yasiyotumia njia za kielektroniki na miundombinu isiyo rafiki katika
kukidhi ushindani wa kibiashara katika bandari hiyo.
Waziri Mbarawa ameitaka TPA
kuweka mfumo wa uendeshaji vikao kwa njia ya kieletroniki (video
conference) kwa lengo la kudhibiti matumizi ya fedha nyingi zilizokuwa
zikitumika katika uendeshaji wa vikao hivyo.
“Nataka TPA muanze kutumia video
Conference katika vikao vyenu ili fedha zilizokuwa zikitumika zifanyie
kazi nyingine za maendeleo ya Taifa”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa TPA imekuwa na
wajibu mkubwa wa kuchangia pato la Taifa kupitia huduma za upakiaji na
upakuaji wa mizigo hivyo wanapaswa kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki
katika ukusanyaji wa mapato katika bandari zote nchini ili kudhibiti
upotevu wa mapato.
“Tukianzisha mfumo wa
kielekroniki katika bandari hii tutakuwa na uwezo wa kufuatilia mapato
yanayopatikana katika utoaji wa huduma na kujua kama malengo
yamefikiwa”, amesema Prof. Mbarawa
Katika Hatua nyingine Profesa
Mbarawa amekagua barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port yenye urefu
wa KM 112 inayojengwa kwa kiwango cha Lami na kumtaka Mkandarasi wa
barabara hiyo China Railway 15 Bureau Group Corporation kukamilisha
ujenzi huo ifikapo Julai mwakani.
Amesema kukamilika kwa barabara
hiyo kutaunganisha mji wa Sumbawanga na Bandari ya Kasanga na hivyo
kurahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka
bandarini hapo na hivyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi katika Mikoa
ya Nyanda za Juu Kusini.
“Kukamilika kwa barabara hii
kutawawezesha wananchi kusafirisha bidhaa zao, kutoka sehemu moja hadi
nyingine na hivyo kukuza uchumi wao na kuongeza pato la Taifa”,
amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa amemuhimiza
Mkandarasi huyo kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyopo katika
mkataba na kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi huo ili kuwezesha
barabara hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara
Nchini, Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina amesema kuwa ujenzi wa barabara
hiyo umekamilika kwa asilimia 62 ambapo kukamilika kwa ujenzi huo
utatagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 133.
“Mpaka sasa Mkandarasi ameweza
kukamilisha kujenga makalvati makubwa 11 kati ya 13, na makalvati ya
kawaida 169 kati ya 241”, amesema Eng Mkina.
Waziri Prof. Mbarawa yupo katika
ziara ya kukagua miradi ya miundombinu na kuangalia utendaji kazi wa
taasisi zilizopo katika Mkoa wa Rukwa.
No comments:
Post a Comment