Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa na wasanii wa filamu
Serikali ya Tanzania inajipanga kuiandikia barua serikali ya India kuomba wataalam wa filamu na muziki ambao watakuja kutoa darasa kwa wasanii wa Tanzania.
Akiongea na Bongo5 Jumapili, Katibu wa Makamu wa Rais, Waziri Rajab Salum amesema yeye kama mwakilishi wa Makamu wa Rais, amelipokea ombi la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, la kuiandikia barua serikali ya India kuomba wataalum watakaotoa mafunzo kwa wasanii wa muziki na filamu.
“Ofisi ya Makamu wa Rais ipo kwa ajili ya kusupport shughuli mbalimbali za nchi, lakini kama ulivyomsikia Mkuu wa Wilaya Kinondoni alivyozungumzia namna gani anaweza kuwasaidia wasanii na kama unavyofahamu mweshimiwa, Samia Suluhu Hassan amefanya kazi na wasanii muda mrefu sana kwenye kampeni na moja ya ahadi zake nikuwasupport wasanii,” alisema Waziri.
“Kwa hiyo kwenye swala la kuwasaidia wasanii kama ofisi ya makamu wa rais sisi tutatia mkono wetu katika kuwasupport wasanii wetu. Kwa sababu ni wasanii wa Tanzania wanatakiwa wasaidiwe na viongozi wa Tanzania, kwa hiyo kama Ofisi ya Makamu wa Rais, tutamsapport Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa support yoyote ile. Kwa mfano amezungumzia pale anataka waalimu kuja kufundisha wasanii wetu wa filamu na muziki, kwa hiyo sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais tutasaidia kama wakileta barua na sisi tutaiandikia India barua ya kuomba wataalam ili waje kufundisha,”
No comments:
Post a Comment