. Rais John Magufuli amewaonya baadhi ya walimu walioanza kuandika idadi hewa ya wanafunzi ili wapewe fedha za ziada akitaka waachane na mchezo huo wa kujitafutia matatizo.
Akizungumza na wananchi wa Kata za Katoro na Buseresere mkoani Geita, Rais Magufuli amewataka wakurugenzi, wakuu wa wilaya na watendaji kuwa na idadi sahihi ya wanafunzi waliopo shuleni.
Amesema kiongozi ambaye hawezi kuwa na idadi ya wanafunzi wote katika wilaya yake atambue hatoshi katika nafasi yake.
Mikoa mipya
Dk Magufuli anayeendelea na safari yake kwenda mapumzikoni Chato, amesema hana mpango wa kuongeza wilaya wala mkoa mpya na anachotaka ni kuwaletea maendeleo kwa wananchi.
Amewataka wabunge wenye nia ya kuomba wilaya, halmashauri au mkoa wasijisumbue kwa kuwa hana mpango wa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment