Monday, 1 August 2016

Mrema amedai anashangazwa na Lowassa kuing’akia Serikali nyakati hizi wakati angeweza kuishutumu wakati ule upinzani ulivyokuwa na nguvu zaidi.

 
Mwenyekiti wa Parole na Chama cha TLP, Augustine Mrema, amesema mwaka 1992 aliwahi kumshauri aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa kukihama chama cha mapinduzi CCM akagoma akidai anataka kula kwanza.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Mrema amedai anashangazwa na Lowassa kuing’akia Serikali nyakati hizi wakati angeweza kuishutumu wakati ule upinzani ulivyokuwa na nguvu zaidi.


“Nilimwambia maji yamechemka tutoke sasa, tukiweka unga tutapata Ugali ukagoma Lowassa, ukasema unataka ule kidogo, ukaendelea na CCM mpaka ulipotaka kugombea Urais akakataliwa na wenzake” Alisema.
Katika hatua nyingine, Mrema amewataka waendesha Boda boda kutoshughulika na maandamano ya vyama vya siasa kwani hayana atija na faida kwao.

No comments:

Post a Comment