Thursday, 3 March 2016

Waziri Nape Nnauye mgeni Rasmi Tamasha la Pasaka Jijini Mwanza

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam wakati alipotangaza jina la mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka mwaka huu litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambaye ni Mh. Nape Nnauye Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , amesema Mh. Nape Nnauye amelipa heshima tamasha la pasaka na amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo jijini Mwanza, Msama amemshukuru Waziri Nape kwa kumtambua mungu na kushiriki katika kazi hiyo ya Mungu siku ya tarehe 27 mwezi Machi mwaka huu.

Akiongelea waimbaji ambao tayari wamethiitisha kushiriki katika tamasha hilo amewataba baadhi kuwa ni Upendo Nkone, Faustine Munishi, Ephraim Sekereti kutoka Zambia, Rose Muhando Jesca BM , Bony Mwaiteje na wengine wengi.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es salaam.
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza  jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es salaam.

Wakuu wa Mikoa wapewa jukumu la kutoa vibali vya kuchangia Elimu

01


Serikali imeongeza wigo wa utoaji wa kibali cha uchangiaji wa elimu msingi bila malipo hadi kwa Wakuu wa Mikoa baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zilizowekwa zimefuatwa kikamilifu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa awali vibali hivyo vilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pekee ikiwa na lengo la kudhibiti michango holela.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa azma ya Serikali ya kutoa elimu msingi bila malipo haizuii wadau mbalimbali wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ambapo wadau wakiamua kuchangia kwa nia ya kushughulikia kero fulani iliyopo katika shule yao au shule zao baada ya kupata kibali wanaruhusiwa kufanya hivyo.

Katika kutekeleza dhana ya utoaji wa elimumsingi bila malipo, hadi kufika mwishoni mwa mwezi Januari, 2016   Serikali inatoa elimu hiyo kwa jumla ya wanafunzi 9,771,902.
Kati ya wanafunzi hao, 8,301,759 ni wa elimu ya msingi na 1,470,143 ni wa sekondari ambao wanapatiwa elimumsingi bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Serikali inasisistiza kuwa viongozi wanahusika katika kusimamia utekelezaji wake ambapo kwa upande wa wazazi au walezi, kamati na Bodi ya shule pamoja na jamii wao nao wanajukumu la kuelewa majukumu yao ipasavyo.

Aidha, juhudi za makusudi zinapaswa kufanywa na viongozi na watendaji wa elimu ili kuwezesha jamii kufahamu wajibu wao katika utekelezaji wa elimumsingi bila malipo na hatimaye kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Katika kutekeleza wajibu wake, Serikali ya Awamu ya Tano (SAT) kuanzia mwezi Januari, mwaka huu imeanza kutoa elimumsingi bila malipo imetoa waraka wa Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 ambao unaofafanua na kubainisha majukumu ya serikali na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa elimu msingi bila malipo.

RC DAR ES SALAAM APIGA MARUFUKU UTOAJI WA VIBALI VYA MALORI YA MIZIGO YENYE UZITO WA ZAIDI YA TANI 10 KUINGIA KATIKATI YA JIJI.

SAD1
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kwa mwaka 2016. Kulia ni Zungu Azzan na Kushoto ni Bw. Edward Otieno Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo.
SAD2
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Isaya Mngurumi akichangia jambo kuhusu uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika Manispaa yake wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam.
SAD3
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akichangia jambo wakati wa wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016.
SAD4
Baadhi ya Wabunge wa jiji Dar es salaam wakifuatilia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mhe. Bonnah Kalua – Mbunge wa Segerea, Mhe. Faustine Ndugulile – Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Zungu Azzan – Mbunge wa Ilala na Mhe. Abdallah Mtolea – Mbunge wa Temeke.
SAD5
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam Muhandisi Julius Ndyamkama akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam kuhusu miradi ya ujenzi wa Barabara inayosimamiwa na Wakala hiyo.

Na. Kalonga Kasati
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki amepiga marufuku utoaji wa vibali vya malori ya mizigo na magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia katika barabara zote zinazosimamiwa na Manispaa za jiji la Dar es salaam zilizojengwa kwa kiwango cha lami kufuatia barabara hizo kuharibika kwa kipindi kifupi kutokana uzito jambo linaloisababishia Serikali hasara.
Aidha, ameziagiza manispaa za jiji hilo kuweka alama za barabarani zinaonyesha zuio kwa magari Yote yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kupita kwenye barabara hizo ili wamiliki na madereva watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka 2016 Mhe. Sadiki Meck Sadiki amesema kuwa Manispaa za jiji hilo zinatenga Fedha nyingi za kujenga barabara mpya na kufanya matengenezo ya zile zilizopo ambazo nyingi zinaharibiwa na malori ya mizigo.

Amefafanua kuwa Matumizi hayo Mabaya ya Barabara kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na Ukiukwaji wa sheria za Barabarani ambapo Malori Makubwa ya Mizigo huegesha na kuziba maeneo Ya Waenda kwa Miguu Jambo linalowanyima haki Wananchi kutumia Maeneo Yaiyotengwa kwa ajili yao.
Amesema Baadhi ya Magari yenye Uzito wa tani 40 hudiriki kupita kwenye barabara za huduma (Service road), Madaraja na wakati mwingine maeneo ya waenda kwa miguu jambo linalosababisha Uvunjaji wa kingo za barabara na milingoti ya taa za barabarani na kuongeza kuwa Vitendo hivyo Vinaisababishia Serikali Hasara kutokana na Gharama ya Matengenezo.

“Kuanzia leo katika Mkoa Wangu ni Marufuku kutoa vibali vya Magari yenye Uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia kwenye barabara zetu, tunataka Barabara zetu zidumu, hatuwezi kuvumilia vitendo vya Watu Wachache wanaokiuka Sheria za barabarani kuharibu barabara zetu, lazima tuchukue hatua Manispaa zinajitahidi kujenga Bararaba lakini hazidumu” Amesisitiza Mhe. Sadiki.

Amesema barabara zinazosimamiwa na Manispaa za Dar es salaam zina uwezo wa kuhimili uzito Wa Tani 10 na kubainisha kuwa kwa kipindi kirefu malori ya Tani 40 yamekuwa yakipita kwenye Barabara hizo na kuzifanya manispaa kunajenga barabara hizo kila mwaka.

Mhe. Sadiki amesema kuwa ipo haja ya mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara katika jjiji la Dar es salaam kwa kuwatumia wataalam wa sheria kuanza kuangalia uwezekano wa Wamiliki wa vyombo vinavyosababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara kulipa gharama za Uharibifu huo.
Kuhusu Ulinzi na Usalama watumiaji wa barabara za jiji amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuchukua Hatua na kufanya Operesheni dhidi ya madereva wa pikipiki (Bodaboda) na Bajaji Wanaopitisha vyombo vyao vya Usafiri kwenye njia za Waenda kwa Miguu na kusababisha usumbufu na ajali za mara kwa mara kwa wananchi wanaotumia njia hizo.

Pia amezitaka Manispaa za jiji hilo kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es salaam kusimamia maeneo yote yanayotakiwa kujengwa miundombinu ya Barabara ili Yasivamiwe na wananchi pamoja na kuwachukulia hatua wananchi wanaofanya biashara katika Maeneo yasiyoruhusiwa ya hifadhi za barabara na njia za waenda kwa miguu.
‘‘Ninaiagiza manispaa ya Kinondoni kuondoa wafanyabishara wote walioko eneo la kituo cha kuzalishia umeme Ubungo, eneo lile ni hatari kwa usalama na maisha yao, kukaa pale ni kinyume cha sheria’’ Amesisitiza.

Aidha, amesema mwaka 2016 mkoa wa Dar es salaam umetenga jumla ya Shilingi bilioni 343.5 ikilinganishwa na Shilingi Biliobi 266.6 zilizotengwa  mwaka 2015/2016 kutekeleza ujenzi na Matengenezo ya Barabara katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari.

Kuhusu Kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016 amesema pamoja mambo mengine kimepokea na kujadili tarrifa  utekelezwaji wa ujenzi wa Miradi ya barabara kwa mwaka 2015/2016 pamoja na kupokea Mpango wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2016/2017.

Ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kuzingatia usafi wa mazingira kwa kulinda Miundombinu ya Barabara na kuepuka kutupa taka kwenye  mifereji  ya kupitisha maji ili kuzuia Mlipuko wa magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.

Tuunge mkono haki sawa na ushiriki wa wanawake katika maendeleo.

02
Na Tabu Mullah
Watanzania na wadau wa Haki za wanawake nchini Wameshauriwa kuunga Mkono Haki sawa na Ushiriki kwa wanawake katika fursa za Uongozi wa kisiasa na kiuchumi na kupima Mafanikio Yaliyofikiwa na kuweka Mipango yenye Matokeo Makubwa. 
Akitoa Taarifa Juu ya Siku ya wanawake Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Wanawake Bi Sihaba Nkinga amesema kuwa Siku ya Wanawake Duniani Husisitiza kujenga Mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha Jamii kutafakari kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku  hiyo ya kila Mwaka.
Amesisitiza kuwa Wananchi Wametakiwa  pia  kubainisha Shuhuda za wanawake Waliotoa Mchango Uliotukuka katika kuwezesha Maendeleo ya Wanawake na Taifa kwa Ujumla na Tafakuri Hii Hufanywa kwa kuelimisha jamii kuhusu Jitihada Mbalimbali zilizofanywa na Serikali Na Asasi Mbalimbali yakiwemo Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake Na kuhamasisha Jamii kuhusu utekelezaji wa sera na Mipango Mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo kwa Wanawake kwa Ujumla.
“Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha Uamuzi kuwa, Maadhimisho Haya yafanyike Kitaifa kila Baada ya Miaka Mitano ili kutoa Muda wa Utekelezaji wa Maazimio na kupima Mafanikio Yaliyofikiwa katika kipindi cha Miaka Mitano”Alisema Bi Sihaba.
Sihaba Nkinga amewashauri Wanahabari Wote kuelimisha Jamii kuhusu kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake kwa Mwaka 2016 inayosema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”, ambapo Kauli Mbiu hii inasisitiza kuwa na Mikakati Thabiti yenye Mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 Yenye Malengo ya kufikia asilimia 50 kwa 50 ya Ushiriki wa Wanawake na Wasichana katika Nyanja zote za Maendeleo.
Aidha Bi Sihaba Nkinga Amemtaka kila Mtanzania aweze kutambua Jukumu alilonalo katika kufikia lengo la Ushiriki Sawa wa Wanawake na wasichana katika Uchumi; Afya, Elimu, Ajira, Sheria na Siasa ifikapo Mwaka 2030.
Kwa mwaka  2016, katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani,mikoa yote Nchini itazingatia Hali na Mazingira ya Mikoa husika na kwa  Mkoa wa Dar es Salaam Siku hii itaadhimishwa  katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa Mikoa yote kuhamasisha Wananchi na Wadau Wote kushiriki Maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia Ujumbe wa kauli Mbiu ya Mwaka 2016.

Wednesday, 2 March 2016

Halima Mdee (Kawe) na Mwita Waitara (Ukonga) na Makada Wengine Watatu Wafikishwa Mahakamani Leo

 
 
Na Kalonga Kasati

Mbunge wa Kawe Halima Mdee na wenzake wanne  wamefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa  shitaka moja la kumjeruhi katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam

Halima Mdee akiwa na mbunge mwenzie Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga  Pamoja na makada wengine watatu wa Chadema  wamekana shitaka hilo na wametakiwa kujidhamini wenyewe kwa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kila mmoja.

Mahakama hiyo imewaachia kwa Dhamana baada ya kuweza kujidhamini

Waziri Mkuu aagiza Watumishi Wote Wahamie Busega

bus9
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua  ujenzi wa wodi ya Wazazi   katika kijiji cha Nyashimo  wilaya ya Busega akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Busega, Dkt, Raphael Chegeni na Kulia nI Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi na watendaji wote wa Serikali wahamie yalipo makao makuu ya wilaya ya Busega kuanzia sasa ili kuleta kasi ya utendaji kazi kwenye wilaya hiyo ambayo ni mpya. 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Machi 2, 2016) wakati akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya siku sita ya mkoa huo atakagua shughuli za maendeleo na kusalimia na wananchi katika wilaya zote za mkoa huo.

“Leo nimeagiza watumishi wote wa umma katika wilaya hii wahame kutoka Magu ambako wanaishi hivi sasa na wahamie hapa Busega ili wafanye kazi kutokea hapahapa. najua kuna changamoto ya nyumba za watumishi lakini waje waishi kwenye nyumba za kupanga wakati Serikali ikiendelea kushawishi NHC, NSSF na Mwananchi Housing Corporation waje wajenge nyumba za watumishi kwenye halmashauri mpya,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kitendo cha watumishi kuhamia yalipo makao makuu ya wilaya kitasaidia kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwani watakuwa wanaziona changamoto zilizopo mahali wanapoishi.
Alisema Serikali inao wajibu wa kujenga ofisi na nyumba za watumishi na kuwahakikishia kuwa azma hiyo itatimia kutokana na makusanyo ambayo Serikali imekuwa ikiyafanya hivi sasa ikilinganisha na siku chache zilizopita.

Jengo hilo la Halmashauri lililoanza kujengwa Julai 20, 2015 litagharimu sh. bilioni 4.66/- na linatarajiwa kukamilika Januari 20, 2017.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Busega, Bibi Gaudensia Bamugileki alisema changamoto kubwa inayowakabili ni kutopatiwa fedha kwa wakati hali ambayo alisema kama itaendelea itaathiri ukamilishaji wa jengo hilo kwa wakati.

“Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa sh. milioni 600. Fedha ambazo zinahitajika kukamilisha ujenzi ni sh. 4,064,580,238/-. Tunaendelea kukumbushia fedha za ujenzi kutoka Serikali kuu ili tupunguze gharama ya kodi inayolipwa kwa jengo la kukodi ambalo pia halitoshelezi mahitaji ya vyumba vya ofisi kwa watendaji na watumishi wa Halmashauri,” alisema.

Katika mkutano mwingine, mara baada ya kukagua wodi ya akinamama, Waziri Mkuu alizungumza na wakazi wa Nyashimo ambako wodi hiyo inajengwa na kuwahakikishia nia ya Serikali kufikisha huduma bora kwa wananchi.

Alitoa shukrani kwa ubalozi wa Japan kwa kuchangia ujenzi wa wodi kwa gharama ya dola za marekani 80,000 pamoja na nyongeza ya sh. milioni 312.1. Pia aliishukuru taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ambayo tayari imejenga nyumba 10 za watumishi kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Busega.

Pia alisisitiza elimu kwa watoto wa kike na kumtaka Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Paul Mzindakaya afanye msako wa kubaini wale wote ambao hawajaanza kidato cha kwanza hadi sasa. “Serikali inataka watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wawe wameripoti shuleni. DC wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hii. Fuatilia na kuwachukulia hatua wote waaliozuia watoto hawa wasiende shule,” alisema.

“Suala la ulinzi kwa watoto wa kike hivi sasa ni la lazima. Ni lazima tuhakikishe mtoto akianza shule ya awali anaingia darasa la kwanza lazima amalize darasa la saba. Akiingia kidato cha kwanza, ni lazima amalize kidato cha nne, akiingia kidato cha tano ni lazima amalize kidato cha sita,” alisisitiza huku akishangiliwa.

Mapema, akitoa taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Simiyu, Bw. Elaston aliomba kuongezewa ukomo wa bajeti ya mkoa kwa mwaka kwa sababu mkoa huo ni mpya na una changamoto nyingi ikilinganishwa na mikoa ya zamani ambayo haina mahitaji ya miundombinu.
“Mkoa wa Simiyu umetengewa ukomo wa bajeti sh. 1,117,133,000.00 wakati mikoa ya zamani kama Morogoro imetengewa sh. 2,836,225,000.00, Arusha (2,595,571,000.00), Kilimanjaro (2,543,463,000.00) Mbeya (2,141,239,000.00) na Tanga (2,318,545,000.00). Tunaomba tufikiriwa ili tuweze kuimarisha miundombinu ya ofisi, barabara, na huduma za jamii katika mkoa huu,” alisema.

MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA, YAWAPIGA MSASA WANAHABARI KUHUSU EL-NINO NA ATHARI ZAKE.

mz
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
…………………………………………………………………………………

Katika Warsha hiyo, Taasisi mbalimbali pamoja na Wanajamii, zimehimizwa kutumia taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo.
 
Pia Wanahabari ambao ni kiunganishi Muhimu katika upashanaji wa habari, wametakiwa kutumia nafasi yao katika kutoa taarifa hizo kwa wananchi ikizingatiwa kwamba, taarifa za utabiri wa hali ya hewa zikiwafikia walengwa kwa wakati, husaidia kujikinga na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Mafuriko na ukame.
 
Warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kwa ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) ikiwa ni katika mpango wake wa Kidunia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa ujulikanao kama Global Framework For Climate Services (GFCS).
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Ziwa, Augustino Nduganda akitoa neno la Shukrani baada ya Ufunguzi wa Semna kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini.
 
 Wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa nchini, Hamza Kabelwa, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
Alphonce Tonny kutoka Metro Fm Mwanza (Kushoto) akiwa pamoja na Iman Hezron Kutoka City Fm Mwanza.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza

Serikali Yaahidi kuwapatia Vijana Mitaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa

xc1
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya kilimo Cha mbogamboga toka kwa Mwenyekiti Kinondoni Saccoss Neema Urio (Kulia) katika ufunguzi Mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kulia mwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana ni Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga na kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
xc2
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya matumizi ya jiko linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa Tanzania Agriculture Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
xc3
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (mwenye koti la Draft) akitoa ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring wa Sinza Dar es Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
xc4
Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki (Hawapo pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
xc6
Baadhi ya vijana wakimsikiliza mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo cha kisasa kwa vijna katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na kushirikisha vijana toka Dar es salaam na pwani.
xc7
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John akitoa neno la Shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tatu Jijini Dar es salaam.

Na Tabu Mullah
Katika kuboresha na kuongeza  ajira  hapa nchini Serikali imeahidi kuwapatia  Vijana  mtaji na Maeneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa ili waweze kujiendeleza na  kukuza kipato chao.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha “Green Houses” Mkurugenzi Wa Maendeleo ya Vijana  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi,  Ajira na watu Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi  amesema  kuwa ni wakati muafaka  kwa vijana kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuwawezesha kupata mikopo kwa riba nafuu na kutoa elimu kuhusu kilimo bora  cha kisasa ili kuondoa fikra zilizopo kwa vijana kuwa kilimo ni kwa ajili ya Watu waliokosa Elimu,wenye Maisha duni na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Ni lazima tutumie fursa Zinazojitokeza katika kunufaika,nina imani mtatumia fursa hii kwa Manufaa yenu na Elimu Mtakayopata itawasaidia kuzalisha bidhaa bora na kuondoa utegemezi. Alisema Mkurugenzi Kajugusi”.

Aidha mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw Praygod Mushi amewataka vijana hao kuamini kuwa kilimo kinaweza kubadilisha maisha yao  kama watatumia fursa zote zinazojitokeza  katika sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.
Naye mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bi Jasmini John ameishukuru Serikali kwa kuaandaa mafunzo hayo na kusema kuwa atatumia elimu atakayopata kuendeleza kilimo kama ajira kwa kutumia pembejeo za kisasa atakazoelekezwa katika mafunzo hayo.

Mafunzo ambayo vijana hao  wamepewa  ni  Jinsi ya kutumia dawa na mbegu bora katika kilimo,kunufaika  na mazao yatokanayo na kilimo cha Green House,utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati ya mwanga wa jua pamoja na ubunifu wa shughuli  za vijana katika jitihada za kukuza viwanda  kwa kutumia mali ghafi za humu nchini.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu kuanzia leo na yameshirikisha vijana kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

BMT kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani kwa Kushiriki katika Michezo.

BMT1
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bi. Zaynab Matitu akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5 mwaka huu ili kuadhimisha siku  ya  Wanawake Duniani  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa wa Baraza hilo Bw. Diomiz Malinzi.
BMT2
Mwenyekiti wa wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Diomiz Malinzi akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5 mwaka huu ili kuadhimisha siku  ya  Wanawake Duniani  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kulia ni Makamu Mwenyekiti Bi. Zaynab Matitu.

DK. AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOKWEPA KULIPA KODI

MPA1
Na Chrispino Mpinge
WAZIRI wa Fedha na Mipango , Dakta Philipo Mpango, amesisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi zao kwa wakati  na kuwaonya wale wote ambao watakwepa  watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria ili kuboresha huduma za jamii na maendeleo ya taifa.
Alisema kuwa serikali  mkakati wa serikali ni  ni kuongeza makusanyo na kulinda utulivu wa uchumi ukuaji wake kwa kasi zaidi  kwa kuwa wafanyabiashara ndio injini ya chumi wa taifa.
Alisema nchi yetu ina utajiri mkubwa wa raslimali ila bado nchi ni masikini  akasisitiza umuhimu wa kila mmoja kulipa kodi na kuwahakikishia kuwa  serikali  haitamuonea mfanyabiashara yeyoyte  na badala yake kutajengwa mazingira ya kuwawezesha kulipa kodi bila usumbufu.
Ametumia fursa hiyo kuwaonya wafanyabiashara ambao wanashirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato TRA, ambao sio waadilifu kukwepa kodi watatumbuliwa majipu
Alisema serikali itanunua mashine za EFD na kuzigawa kwa wafanyabiashara wote bure lengo ni kuhakikishia zinatumika katika manunuzi na mauzo ya bidhaa kwa ajili ya kutolea risti kwa mununuzi.
Amesema lengo la kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu  wa kulipa kodi ili kujenga Tanzania mpya yenye  uchumi wa viwanda,na hiyo ndio vipaumbele vya mwaka wa fedha  2016/17.
Alisema atafuta kodi zote ambazo ni kero na tayari wizara imeshaziandikia wizara zingine na halmashauri  kuainisha kodi zenye kero ili zifutwe kwenye bajeti ijayo.
Wakichangia kwenye kikao hicho wafanyabiashara wameihakikishia serikali kuwa watalipa kodi ila wanataka kushirikishwa kwenye utungaji wa sera .
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,amesema mkoa wa Arusha unakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za sekta ya madini  kuwa na makusanyo kidobo kutokana na madini kutoroshwa kwa kupitia mpakani kutokana na eneo la mpaka kuwa kubwa mno.
Waziri alikuwa akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha ili kuwasikiliza kero zao ambazo zinasababisha kodi kutokulipwa ipasavyo na hivyo kuikosesha serikali mapato.

Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi Tamasha la Wanawake

tm1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi. Agnes Mgongo (katikati) akiongea na waandishi wa  habari kuhusu   tamasha  la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kushoto kwake ni Mratibu wa tamasha hilo Bi. Anawery Phares na kulia  ni  mshehereshaji (MC Pilipili) Bw. Emanuel Mathias.
tm2
Mratibu wa Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016 Bi. Anawery Phares(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan,Kushoto ni Mwanamuzi wa Taarabu Bi. Patricia Hillary na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Bi.Agnes Mgongo.
tm3
Mchekeshaji na Mshehereshaji  Bw. Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili akito kionjo cha mojawapo ya kichekesho atakachokifanya siku ya tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016,kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Agnes Mgongo na kulia ni Mwakilishi wa Children Survial Hut Tanzania (CSI) Bi.Stella Mranda.
tm4
Msanii wa Muziki wa Taarabu Nchini Bi .Patricia Hillary akieleza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  kwa tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Na Kalonga Kasati

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika Machi 5, 2016.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Agnes Mgongo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa King Solomoni uliopo Nanga jijini Dar es salaam kwa kujumuisha jinsia zote .
Ameongeza kuwa Kampuni ya Trumark imeandaa tamasha hilo kwa lengo la kuwahamasisha Wanawake kuwa na nguvu katika nafasi ya kuchangia na kuinua uchumi na maendeleo ya nchini.
“Ni kweli wapo wanawake wenye mafanikio lakini  kuna changamoto zinawakabili  ikiwemo Uchache wa ushiriki wa wanaume katika kufanikisha mafanikio ya wanawake na kufungua fursa ili waweze kuwa sehemu ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii” alifafanua Agnes.

Mbali na hayo Bi. Agnes amesema kuwa kila mtu kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu Ya Maendeleo, hivyo kila mtu na mahali popote alipo ashiriki vyema kutimiza wajibu wake huku wakishirikiana na kusaidiana kwa pamoja ili kujenga taifa.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya Watoto na wanawake  (CSI Tanzania) nchini Stelala Mranda amesema kuwa  wameahidi kuwawezesha wanawake 20 watakaotaka kuhudhuria tamasha hilo.
Wadau mbalimbali wakiwemo Marie stopes Tanzania, CSI Tanzania, wamejitokeza kudhamini tamasha hilo lililobeba kauli mbiu isemayo “Pamoja tutafanikisha”.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa Njia za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani  ya mlango wa uzazi kwa washiriki na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa Njia za Uzazi wa Mpango, Upimaji wa saratani  ya mlango wa uzazi kwa washiriki na wananchi wote Watakao hudhuria tamasha hilo.

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ashiriki Mkutano wa 17 wa EAC Arusha

SEN2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha Palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,[Picha na Ikulu.]
SEN3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,[Picha na Ikulu.]
SEN4
Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha,[Picha na Ikulu.]
SEN9
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC  uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo,{Picha na Ikulu.]

Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Kenyatta na Rais Kagam

SEN1
Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki akiwemo mwenyekiti wa mkutano wa 17 wa EAC Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa Mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ngrdoto Mkoani Arusha,[Picha na Ikulu.]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.
Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.
Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.
“Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana” Amesisitiza Rais Kenyatta.
Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.
Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi Mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo” amebainisha Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga Mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.
Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa Umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.
Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.
Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha
02 Machi, 2016

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe anastazia Wambura azidi kupokea Michango ya Timu ya Twiga stars

UR1
Mhasibu wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Godfrey Osmund akimweleza Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura jinsi atakavyozikatia risiti fedha ambazo Wadau wa michezo wamezitoa kwa ajili ya kuichangia Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu ya Twiga Stars.
UR2
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi  leo Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni mbili zilizotolewa na Mohammed Dewji kwaajili ya kuisaidia timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Hadi Sasa wadau wa Michezo Wameshaichangia Timu hiyo shilingi milioni 17.


Waziri January Makamba azindua kamati ya kitaifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa Jijini Dar es salaam

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba  (kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.
 Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za magonjwa yanayolishambulia.
 Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla 
hiyo ya uzinduzi.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa bize wakati wa uzinduzi huo.
 Wajumbe wa kamti hiyo
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi 
Mkutano ukiendelea.
Waziri Makmba (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI. Kutoka kushoto ni  Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru, Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour na Profesa Raphael Chibunda.
Picha ya pamoja na Waziri Makamba.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Makama na wajumbe wa kamati Mpya jinsi maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI inavyofanya kazi.
Mimea mbalimbali inayofanyiwa utafiti ikiwa katika chupa maalumu katika maabara hiyo.
Mbegu ya migomba iliyooteshwa baada ya kufanyiwa utafiti katika kituo hicho cha MARI.

Na Kalonga Kasati
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao na kuisaidia serikali.
Makamba alitoa mwito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
“Tengenezeni mpango kazi wenu ili serikali iufahamu na kuweza kuwasaidia kifedha Endapo utakwama badala ya kukaa bila ya kuwa na dira na kusubiri kufanya Mikutano yenu ya kupitisha jambo fulani mara tatu katika kipindi cha miaka nane” alisema Makamba.
Alisema kamati hiyo ni ya muhimu sana katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya Matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.
Alisema Tanzania ni nchi mwanachama wa mkataba wa bioanuai wenye malengo Makuu matatu,  Hifadhi ya bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yake.
Alisema Tanzania iliridhia mkataba huo mwezi Machi, 1996 ili kushirikiana na Jumuia ya Kimataifa katika kutekeleza malengo yaliyotajwa.
Alisema alisema changamoto kubwa ya teknolojia hiyo ya bioteknolojia ya kisasa Bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea ambazo ni mzio, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani, usugu wa dawa kwa matibabu ya magonjwa, wakulima kutegemea mbegu za kununua kila na madhara mengine ambayo kwa sasa hayajawa bayana.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru alisema wamejipanga kujenga kituo kikubwa cha utafiti kitakacho Gharimu dola za Marekani 556,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda alisema ili wakulima waweze kufanikiwa katika kilimo chao ni vizuri wakawa wanazingatia ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa wakifanya Tafiti mbalimbali ambazo huwapelekea wao kwa matumizi ya kilimo.