Wednesday, 2 March 2016

Waziri Ummy Mwalimu apokea Msaada wa Fedha wa Mil 22o kwa Matibabu ya Wagonjwa wa Moyo

waziri ummy5
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi akisoma taarifa fupi juu ya magonjwa wagonjwa wa moyo wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo na namna walivyojipanga kutoa matibabu ya upasuaji kwa watoto hao 101, waliolipiwa gharama za matibabu kutoka BAPS Charity. Wengine ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa BAPS Charity.
waziri ummy 4
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa wazazi waliokuwa katika tukio hilo la kukabidhiwa fedha kiasi cha Mil 220, kwa ajili ya wagonjwa wa moyo 101, ambao wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika taasisi ya JKCI.
waziri Ummy 2
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kumjulia hali mtoto Zahara Seleman Muna (10) ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amejitolea kama Waziri kuhakikisha atawasaidia watoto hao katika kutimiza ndoto zao ikiwemo kuwasomesha na masuala mengine kupitia Wizara yake ambayo yenye dhamana, Waziri Ummy aliguswa na watoto hao kutokana na ndoto zao walizokuwa nazo ikiwemo kusoma zaidi.
waziri ummy 6
Mwenyekiti wa taasisi ya BAPS Charity, Subhash Patel, akizungumza machache kuhusiana na mchango huo wa Milioni 220, kwa ajili ya matibabu ya watoto 101, ambapo pia aliomba wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikuisaidia Serikali katika kuhakikisha uhai kwa wagonjwa wa moyo hasa watoto hapa nchini.
WAZIRI UMMY MWALI
Bw. Alfred D. Dafi mkazi wa Karatu akiwa amembeba mtoto wake, Beatrice Alfred (13) akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu kwa kuweza kuchukua majukumu ya kumsaidia mtoto wake katika masuala ya kumsomesha na mambo mengine kama Waziri mwenye dhamana. Waziri amechukua jukumu ya kuwasaidia watoto hao, kutokana na kuguswa na ndoto walizonazo ikiwemo kusoma wafike mbali. Mtoto huyo Beatrice hadi sasa anasoma darasa la sita, katika shule ya Sumawe, iliyopo Karatu.
WAZIRI DK
Dk. Naiz Majani, ambaye ni daktari wa watoto wa magonjwa ya moyo akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya matatizo ya magonjwa ya moyoo ambapo amebainisha kuwa kati ya asilimia 10, Pekee magonjwa ya moyo yanabainika kwa mwanamke huku miongoni mwa wazazi wanaozaa Watoto wenye matatizo ya moyo ni wale waliokosa chanjo mbalimbali ikiwemo ya Lubela na mambo mengine.
WAZIRI UMMY 111
Watoto Beatrice Alfred (13) na Zahara Seleman Muna (10) wakiwa katika picha ya pamoja. Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu ameamua kujitolea kuwasaidia kutimiza ndoto zao ikiwemo suala la kuwasomesha na mahitaji mengine kama Waziri mwenye dhamana. Kushoto ni Baba wa mtoto Beatrice, Bw. Alfred Dafi ambaye anatokea Karatu.
WAZIRI UMMY 76
Waziri Ummy Mwalimu akimpa pole dada wa Zahara Seleman Muna (10), Editha Foi,(kulia) Aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya Waziri Ummy Mwalimu kuamua kujitolea kuwasaidia Watoto hao iliwatimize ndoto yao ya elimu na mahitaji mengine kama Waziri Mwenye dhamana.
WAZIRI UMMY 87
Uchungu wa Mama”, Waziri Ummy Mwalimu akiwa na watoto Beatrice na Zahara ambao wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, ambapo baada ya kuwajulia hali na kuguswa na ndoto zao za kielimu, Waziri Ummy Mwalimu ameguswa na watoto hao na kuamua kuwasaidia katika elimu na mambo mengine kama Waziri mwenye dhamana.
waziri ummy 89.Waziri Ummy Mwalimu akiwa akipeana mkono na baada ya kukabidhiwa hundi ya sh. Mil 220, iliyotolewa na taasisi ya BAPS Charity kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto 101, wa magonjwa ya moyo waliopo katika taasisi ya JKCI. 
 
Na Tabu Mullah

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Ally Mwalimu leo Machi 2.2016, amepokea msaada wa fedha kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa Moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa msaada huo, jumla ya Watoto 101, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo kwa gharama za fedha Hizo zilizotolewa na Jumuiya ya Kihindu waishio Dar es Salaam ijulikanayo kama BAPS Charity, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo waliouonyesha kwa watanzania Wanaosumbuliwa na Maradhi ya moyo.

Wiziri Ummy amebainisha kuwa, kiasi cha msaada unaotolewa utawezesha wagonjwa wapato hao kupatiwa matibabu ya moyo hivyo kuwa, faraja kubwa kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiria Huduma hizo kwa muda mrefu kutokana na kushindwa gharama za matibabu yake.
Aidha, kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amepongeza kwa Msaada huo kwani utasaidia kutoa matibabu kwa watoto hao 101, huku pia taaisi yake ikikabiliwa Na changamoto ya wagonjwa wengi ambapo amezitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikupunguza wagonjwa wanaosubiria kupatiwa matibabu hasa upasuaji.

Prof. Janabi ameeleza kuwa, matibabu ya wagonjwa wa moyo yana gharama kubwa kwani kwa Mtoto mmoja ndani ya nchi yanafikia hadi Milioni nne (Mil 4) huku kwa nje ya nchi matibabu hayo Yakifikia hadi Milioni 16, gharama hizo ni kubwa hivyo wadau na taasisi binafsi zimeombwa kujitokeza ilikuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa watoto ambao wapo katika taasisi hiyo na Mikoa mingine.

Tuesday, 1 March 2016

EWURA Yatangaza kushuka kwa Bei ya Mafuta


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 Machi bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2016.
Kwa Machi 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’
‘kwa kiasi kikubwa, kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia

Niabu Waziri Wa Afya Dk Hamis Kigwangalla ameagiza kufungwa Chumba cha Upasuaji Hospitali ya Sanitas Ya Mikocheni

Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali Nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa Mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya Upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba Cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha Mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
dk kigwa
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
dk hk 888
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
dk hk55
Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Kigwangalla akitoa maagizo
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
dk hkna
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya ‘karatasi’ iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
dk kigwa
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
dk hk iio
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
dk hk67
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew

Mahakama ya Tanzania Yakutana na Wadau jijini dar es salaam Yasisistiza Utoaji wa Haki kwa Wakati na Uboreshaji wa Miundombinu

MAHM1
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza
MAHM2
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza
MAHM3
Washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
MAHM4
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia.

Na. Kalonga Kasati
 
Mahakama ya Tanzania imesema kuwa inaendelea na mkakati wa kufanya maboresho ya miundombinu yake ili kurahisisha  utoaji wa huduma ya mahakama kwa wadau na wananchi kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Katanga wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam.

Bw. Katanga amewaambia wadau hao kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya mabadiliko ya huduma zake kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka Serikalini pia kutoka kwa wadau wa Haki wanaoiwezesha Mahakama kufanya maboresho hayo kwa lengo la kukuza Utoaji wa Haki nchini.

Amesema ili kusogeza huduma karibu na wananchi  Mahakama itatekeleza Mpango mkakati wa miaka 5 wa kuiwezesha kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau na Taasisi za utoaji Haki katika masuala yanayohusu shughuli za kila siku za utendaji wa Mahakama nchini.
“ Mahakama tutaanzisha mpango wa miaka 5 ambao utaanzisha mfumo wa wa kushirikiana na wadau wetu kwa karibu katika mambo yanayohusu shughuli zetu ili kuwaondolea wananchi usumbufu na upotevu wa muda pindi wanapofuatilia huduma” Amesema.

Amefafanua kuwa Mahakama imeshaanza kujenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama za Mwanzo katika maeneo mbalimbali  nchini ikiwemo Mahakama ya mwanzo Kigamboni jijini na Kawe zote za jijini Dar es salaam, Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga  na Kibaha mkoani Pwani ili kurahisisha utoaji wa Haki.

“ Mahakama sasa tuko katika mwelekeo mzuri wa kufanya mabadiliko, kwa kushirikiana na wataalam wetu wa ndani wakiwemo Chuo Kikuu Ardhi , tunaendelea kujenga majengo mapya ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Kigamboni, Mkuranga, Kibaha na Kawe ambayo yatakamilika ifikapo Juni mwaka huu” Amesisitiza.

Bw. Katanga ameongeza kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa majengo yaliyopo yanakarabatiwa sanjali na ujenzi wa majengo mapya katika Mahakama zote 133 nchi nzima.
Aidha, amebainisha kuwa Mahakama inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa watumishi wake ikiwemo ununuzi wa mabasi ya kusafirishia watumishi, magari madogo na Pikipiki ili kuwawesha watumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Solanus Nyimbi akizungumza na wadau hao amewataka wafanye kazi kwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza imani yao kwa Mahakama.

Amezitaka Taasisi na wadau wanaohusika na utoaji wa Haki kujikita katika kushughulikia matatizo ya wananchi ili kufanikisha dhana ya Utoaji Haki kwa Wakati ili kwenda na mpango uliowekwa na Mahakama wa kuondoa mrundikano wa mashauri mahakamani na ule wa kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu.

Naye Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza ametoa wito kwa Taasisi za Utoaji wa Haki kukutana mara kwa mara ili kujdili na kutatua changamoto zinazoukabili Utoaji wa Haki nchini.

Kuziona Twiga Stars na Zimbabwe 2000

Kiingilio cha chini cha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Taifa Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake Zimbambwe kitakua shilingi elfu mbili tu.

Mchezo huo namba 3, unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu tatu kwa jukwaa kuuu.
Waamuzi wa mchezo huo ni Lidya Tafesse, akisaidiwa na Yehuzewdubizua Yehuw, Tsige Sisay, Woinshetkassaye Abera kutoka nchini Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo huo Geneviev Kanjika akitoka Congo DR wote wanatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).
Wakati huo huo kikosi cha Twiga Stars kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo wa siku ya Ijumaa, huku kocha mkuu wa timu hiyo Nasra Juma akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kuwakabili Wazimbambwe.
Aidha Kocha Nasra amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini na watanzania wote kwa ujumla, kujitokeza uwanjani siku ya Ijumaa kuja kuwapa sapoti katika mchezo huo, ambapo watakua wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya Tanzania.

JAFO AMUAGIZA MKURUGENZI WA KISARAWE KUMTAFUTIA KAZI NYINGINE MENJEJA WA MAMLAKA YA BODI YA MAJI

Jafo-30Jan2016
Na Tabu Mullah
 NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora,  Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji kwa muda mrefu.

 Jafo ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kisarawe alisema, hawawezi kuendelea kukaa na watumishi ambao hawaguswi na matatizo ya wananchi.
 Alitoa agizo hilo juzi mjini Kisarawe, kwenye mkutano aliouandaa kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa ridhaa ya kuendelea kuongoza jimbo hilo, na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hao.

 Naibu Waziri huyo alimtaka Materu kuachia nafasi ya Meneja ili apangiwe kazi nyingine kwani ameshindwa kutatua changamoto ya maji katika mji wa Kisarawe.
 “Mkurugenzi mtafutie kazi nyingine katika ofisi yako, hatuwezi kuwa na watu ambao hawaguswi na matatizo ya watu tafuta atakayekaimu nafasi yake katika kipindi hiki.
 Hatufanyi mambo ya kuchekeana, na hatuwezi kuibadilisha  Kisarawe yetu kama tutaendelea kuwavumili watumishi wanaochangia kudumaza maendeleo”alisema Jafo.
 Inadaiwa kuwa, Materu amekua meneja wa Mamlaka hiyo kwa zaidi ya miaka kumi lakini hakuna njia mbadala iliyobuniwa na mamlaka hiyo kuondoa tatizo la maji kukosekana mara kwa mara.
 Mji huo wa Kisarawe una chanzo cha maji cha kimani ambacho kinatoa lita 16000 kwa saa na chanzo kingine cha minaki kinachotoa zaid ya lita 10,000 kwa saa hali ambayo ni dhahiri kusingekuwepo na tatizo la  maji.

 Wananchi waliohudhuria katika mkutano huo walifurahishwa na kitendo kilichofanywa na mbunge wao huku wakiendelea kumuomba ahamie katika idara ya ardhi.

 Mwajuma Yusuph, Salehe Ally na Said Issa walisema kitendo cha kuondolewa Meneja huyo kitaleta mabadiliko kwani baadhi ya watumishi wanafanya kazi kwa mazoea bila kujali adha inayowapata wananchi.

Profesa MAYUNGA HABIBU NKUNYA ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)


maxresdefaultWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa Mamlaka aliyopewa amemteua Profesa MAYUNGA HABIBU NKUNYA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuanzia Februari 17, 2016.

Uteuzi huo ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 17 Februari, 2016 hadi 16 Februari, 2019.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Nkunya alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Programu ya Mapitio ya Mfumo wa Taifa wa Ubunifu (National Innovation System Review Programme).

Uteuzi huo unafuatia kumalizika kwa muda wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.  
Taarifa hii imetolewa na,
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI),
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
01 Machi, 2016

Makamu Wa Rais Mhe Samia Suluhu amekamilisha Ziara ya Siku Mkoani

m1
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliangalia vijana wa kikundi cha sanaa cha Tanga kwanza alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.                
m2
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01.2016.
m3
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na vijana wa kikundi cha wasanii cha Tanga kwanza alipokua akiondoka katika Ofisi ya Chama cha  Mapinduzi CCM Mkoa Tanga baada ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016.  (Picha na OMR)        
m4
 Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga Mwanakombo Mwakuru akimvisha Skafu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais  amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga. Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe.Henri Shikifu.
m6
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Tanga katika Ofisi ya CCM Nkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01,2016.
m5
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01.2016.

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kwa Rais Mstaafu Kikwete


halRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kilichotokea leo asubuhi nchini India.
Mzee Selemani Mrisho Kikwete alikuwa nchini India kwa matibabu.

Katika salamu zake Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Mzee Selemani Mrisho Kikwete na amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete kuombeleza kifo cha mtu muhimu kwa familia hiyo.

“Napenda kukupa pole nyingi wewe Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, familia yenu yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika familia, natambua uchungu mkubwa mlionao lakini nawaomba muwe  uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” Alisema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amemuombea Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Arusha
01 Machi, 2016

Wataalamu TPRI Wapelekwa Kilombero kufanya Uchunguzi

dk rutNa Dustan Kamala
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro imewapeleka wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuwatilifu ya Kitropiki (TPRI) wilayani Kilombero kufanya uchunguzi wa zao la mpunga linalosadikiwa kuharibiwa na dawa zilizomwagwa na Kampuni ya Kilombero Plantation (KPL) inayomiliki mashamba yanayopakana na mashamba ya wananchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Morogoro Bw. Ernest Mkongo kuhusu uchunguzi unaoendelea kufanyika katika mashamba ya wananchi ili kutathmini athari zinazotokana na dawa hizo.
“Wataalamu kutoka TPRI wameshafanya uchunguzi wa awali na mpunga huo umeonekana kuwa na rangi ya njano isivyo kawaida, hivyo wamechukua sampuli za mpunga huo na kuzipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kujua kama umeharibiwa na dawa za kuondoa magugu zilizomwagwa na Kampuni ya KPL” alisema Mkongo 
Aidha, Bw. Mkongo ameongeza kuwa, Taasisi ya TPRI ina wataalamu wa uhakika kwa hiyo anaamini watatoa majibu ya ukweli juu ya tatizo hilo.
TPRI ilianzishwa miaka ya 1940 ambapo kwa Tanzania ilirasimishwa rasmi katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria Na. 18 ya mwaka 1979 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa zinazoathiri afya ya binadamu, wanyama na mazao.

Serikali yawapa motisha wachezaji wa Twiga Stars

TWI1
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM
TWI2
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia).
TWI3
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga akitoa shukura kwa Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia wadhamini Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura(wapili kutoka kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge.
TWI4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” (Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a.
TWI5
Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”  Bibi. Nasra Juma  wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.

Na: Chrispino Mpinge
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars) ikishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa tarehe 4 machi katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.

Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake Dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la sh. Laki tatu kama mptisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidi timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mechi ya tarehe 4 machi dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa katika uwanja wa Taifa.

Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake Muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Specila Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga ameipongeza Serikali kwa jitihada Zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Mwesiga pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.

Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmoja aliyechangia sh. Milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS sh. Milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni 10.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akabidhi Michango ya Twiga Stars

wm1
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi  Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Fedha hizo zimewekwa  katika Benki ya NMB Bank House akaunti  namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
wm2
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimsikiliza Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Ijumaa ya wiki hii timu hiyo itacheza na   Zimbabwe  mashindano ya awali ya kufuzu kombe la Afrika kwa wanawake.
wm3
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimweleza jambo   Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha hizo  katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.

Serikali yalitaka Dira ya Mtanzania kukanusha tuhuma Dhidi ya Balozi Ombeni Sefue

mwb1
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la tarehe 29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw.Jamal Zuberi na Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw.Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
mwb2
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw.Assah Mwambane (ambaye hayupo katika picha) iliyokuwa ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha habari waliyoitoa hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu”.


Na Kalonga Kasati
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene ameutaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali na   Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa waliyoitoa katika toleo namba 404  la tarehe 29/02/2016 lenye  kichwa cha Habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu.

Hayo  yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na Waandishi Wa habari kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala kuhusika na kampuni ya CRJE katika utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma Oktoba 2007  kwani katika kipindi  hicho alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

“Serikali inautaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo kwa uzito ule Uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga wakidai wana ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika  ikiwemo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema Bw.Mwambene.

Aidha,  Bw.Mwambene amesema gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipigia chapuo Kampuni ya “UGG”  iliyowahi kuonyesha nia ya kujenga reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya kweli na hakuna kampuni  yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya kujenga reli hiyo.

Mkurugenzi aliendelea kusema kuwa gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati alichokifanya Balozi Sefue ilikuwa ni kusoma Matokeo ya Uchunguzi ambao hakuufanya yeye. Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi huo.

Hata hivyo serikali imewashauri Wamiliki wa vyombo vya habari,wachapishaji,wahariri, na Waandishi wa Habari wajikite kwenye weledi na ukweli pia wafanye  Utafiti wa kina  na kuandika Mambo waliyo na uhakika nayo

Watanzania Wahimizwa kuchangia Damu kwa Hiyari Kuokoa Maisha

 Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na
mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi
la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi
hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la
Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa
wiki.
 Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na
mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi
la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi
hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la
Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa
wiki.
 Mfanyakazi
wa Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kushoto)
akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiyari
wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura
hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa
Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya
kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa
hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la
Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi.
Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa
ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha
Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa vipimo
katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki. 
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.

Na Kalonga Kasati
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kitengo cha Dharura Wametoa Rai kwa watanzania kujitolea kwa Hiyari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa Wanaopokelewa hospitalini hapo.
Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki katika eneo la Karume jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amebainisha kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwani litasaidia kuokoa maisha ya
Wagonjwa wenye uhitaji huo wanaopokelewa hospitalini hapo kama vile
waliopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto.
“Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 lakini Tunafanikiwa kupata wastani wa chupa 40 hivyo kuwepo na upungufu wa chupa 60 kila siku. Hali hii inapelekea kuhudumia
Wagonjwa wenye uhitaji wa dharura tu huku wengine wakisubiri.” Alisema Profesa Maseru
“Wataalamu wananiambia kuwa kwa kawaida, damu inaweza kuhifadhiwa kwa Muda wa takribani mwezi mzima kabla ya muda wake wa kutumika kwisha, na kutokana na uhifadhi wa damu kwa muda mfupi ndiyo maana tunasisitiza Umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara.  Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka.” Aliongezea Profesa Maseru
“Katika wakati wa kutoa huduma ya tiba ya dharura, haswa kwa wagonjwa wa Ajali, watoto na wamama wajawazito, upatikanaji wa huduma ya  Ambulance na damu kwa wakati huongeza nafasi ya
kuishi kwa wahitaji kwa kiasi kikubwa mno na huduma hizi huokoa maisha Ya mamilioni ya wagonjwa kila mwaka duniani kote,” alisema na kumalizia, 
“Natoa rai kwa wakazi wa Dar es slaaam na Watanzania wote kwa ujumla kujenga Utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya damu ya kutosha, kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji damu wa kujirudia Mpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu nchini.”
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif, kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa ving’amuzi kwa ajili ya Matangazo ya dijitali ambao walidhamini zoezi hilo amesema kuwa hii ni mara ya pili wao kudhamini zoezi hilo kutokana
na umuhimu wake katika kuokoa maisha ya watanzania wote kwa ujumla.
“Hakuna asiyefahamu katika maisha yetu yanayotuzunguka ajali zimekuwa nyingi zinazopelekea watu kupoteza maisha maelefu kubaki mejeruhi wenye uhitaji mkubwa wa damu ili kupata matibabu. Kama
tunafuatilia vyombo vya habari basi tutakuwa tunasikia ni mara ngapi kwa Wiki ajali zinatokea barabarani na kuacha majeruhi wengi. Kwa upande wa akina Mama wajawazito wanahitaji damu kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kujifungua. 
Hatuwezi kukaa pembeni na kuwatizama wakikosa msaada wakati uwezo huo Tunao.” Aliongezea Bi. Hanif “Tumejisikia faraja sana kuwa wamojawapo wa wadau walioshiriki kufanikisha zeozi hili na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Muhimbili katika kuwahamasisha watanzania wajitokeze zaidi. 
Kwa mujibu wa wataalamu tunaweza kujitolea damu mpaka mara nne ndani ya mwaka, nina
uhakika kila mtanzania akifanya hivyo basi benki yetu ya damu itajaa na tutaweza hata kusaidia wengine wan chi za jirani wenye uhitaji.” Alimalizia Makamu wa Rais kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania.

Shida ya maji jiji la Dar es salaam kuwa historia

 Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Mhandisi Romamus Mwang’ingo (Kushoto)  akitoa maelekezo kwa Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) juu ya ufanyaji kazi wa mitambo ya Ruvu chini.
 Mafundi wakiwa katika harakati za kulaza bomba litakalotumika kuleta maji kwenye tanki kubwa lililopo kibamba toka Ruvu chini na juu kwa ajili ya uhifadhi na usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam. 
Mafundi wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
 Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Katikati) akisikiliza maelezo juu ya ufanyaji wa kazi wa mitambo inayotumika kusambaza maji toka Ruvu juu kutoka kwa Meneja Mradi toka kampuni ya WABAG Mr. Pintu Dutta wakati wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea mitambo hiyo. 
 Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kushoto) akisikiliza maelezo juu ya ramani inayoonesha usambazaji wa maji toka Ruvu Juu kwenda katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Romamus Mwang’ingo.