Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga
mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17
mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima
kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo akihutubia wakati
wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka
2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi
nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa
Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya
mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo
mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima
kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Viongozi wa NBS, Chuo cha Mipango na baadhi ya
wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17. Utafiti
huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba
na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Oscar Mangula akiwaapisha wadadisi wa Utafiti wa Takwimu
za Kilimo kwa mwaka 2016/17 baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo
mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima
kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Na: Veronica Kazimoto- Dodoma
Serikali kupitia Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/17
nchi nzima kuanzia kesho tarehe 3 Oktoba hadi tarehe 3 Novemba, 2017.
Akizungumza leo wakati wa kufunga
mafunzo ya wadadisi watakaokusanya Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17
mkoani Dodoma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria
Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni kutoa makadirio ya kiasi cha
uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo, mazao yatokanayo na mifugo
na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.
“Ningependa kuwasisitizia
washiriki kuwa, dhumuni kubwa la utafiti huu wa kilimo ni kutoa
makadirio ya uzalishaji wa mazao makuu ya kilimo na maeneo yake
yaliyolimwa pamoja na taarifa za mifugo katika mikoa yote ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania”, amesema Dkt. Mashingo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo ametoa
wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa kushiriki kwenye utafiti
huu, kutoa ushirikiano wa kutosha na hususan kutoa taarifa sahihi kuhusu
hali ya uzalishaji wa mazao, huduma zinazotolewa na Maafisa Ugani na
aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha changamoto wanazokumbana nazo
katika shughuli zao za kila siku.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema jumla ya wadadisi 600
wamepatiwa mafunzo ya siku 5 kwa ajili ya kufanya utafiti huo nchi
nzima.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni kuwajengea uwezo wa kuhoji na
kujaza madodoso ya wamiliki wa mashamba (wakulima) na namna ya kutambua
mahali shamba lilipo kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho GPS.
Utafiti huu wa Kilimo wa mwaka
2016/17 unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya
Mtakwimu Mkuu, Zanzibar (OCGS) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
No comments:
Post a Comment