Uholanzi yaikung'uta Belarus 3-1
Nahodha wa Uholanzi, Arjen Robben akienda chini baada ya kukwatuliwa na
beki wa Belarus, Sergei Balanovich katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe
la Dunia kwa upande wa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Borisov Arena
mjini Borisov. Uholanzi ilishinda 3-1 mabao yake yakifungwa na Davy
Propper dakika ya 24, Arjen Robben kwa penalti dakika ya 84 na Memphis
Depay dakika ya 90 wakati la wenyeji lilifungwa na Maksim Volodko dakika
ya 55.
No comments:
Post a Comment