leo Oktoba 1, 2017 siku ya wazee duniani Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni imewapatia vitambulisho vya matibabu bure Wazee 2530, sawa na asilimia 60 ya wazee 4166 waliotambuliwa huku kati yao Wanawake wakiwa 1838, Wanaume 2328.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameeleza kuwa licha ya kuwapatia vitambulisho hivyo, amesema imewekwa mikakati maalumu ya kutambua changamoto nyingine za wazee ili waweze kuwawezesha wazee hao, ambapo pia amewashuri wajiunge katika vikundi ili iwe rahisi kuwafikia
Akisoma risala hiyo kwaniaba ya Wazee kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Nassoro Juma Mataula wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kuwapatia kadi za matibabu kwakuwa wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wengine hadi kupoteza maisha
Maadhimisho ya sikuu hii katika wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam yamefanyika Mwananyamala katika kata ya mkumbusho, na kitaifa yamefanyika Katika mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment