MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na
kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya
mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee
jijini hapa.
Ugeni huo uliwakilishwa na, Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya
Afrika Hastings Chikoko, Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia
kutoka Nchini London.
Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo, Meya Mwita
amesema kuwa wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha
miundombinu yenye changamoto ya mafuriko,joto ili wananchi waweze
kuepukana na kadhia hiyo.
Amefafanua kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuleta mtalamu wa
masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambaye atafanya kazi ya
kushughulikia changamoto mbalimbali zinazo husiana na masuala ya
mabadiliko ya tabia ya nchini jijini hapa.
Amesema mbali na hilo lakini pia wameahidi kutoa fedha kwa ajili ya
kuboresha maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko ikiwemo bonde la mto
msimbazi, Jangwani na maeneo mengine.
Amesema jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na changamoto kubwa
ya mafuriko kipindi cha mvua jambo ambalo husababisha baadhi ya wananchi
kupoteza maisha, hukuwengine wakikumbwa na uharibifu mkubwa wa mali
zao.
“ Leo nimekutana na marafiki zetu hawa wa C40 CITIES, tumeongea mambo
mengi, lakini ya kujenga na kuliletea jiji letu maendeleo katika sekta
ya miundombinu ambayo imekuwa ni changamoto katika jiji letu,
nimewapokea na ninawakaribisha sana”.
“ Mji wetu unakuwa kwa kasi kubwa, tunatakiwa kujipanga mapema, maeneo
mengi yanakumbwa namafuriko wakati wamvua , wananchi wetu wanahangaika,
sasa imefika kipindi ambacho tunapaswa kulipatia ufumbuzi jambo hili”
amesema Meya Mwita.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings
Chikoko,amesema kuwa wamekuja jijini hapa kwa ajili ya kusaidiana katika
maeneo matatu ambayo ni usafiri jijini,mafuriko na ukame ili kuwezesha
kilimo cha mijini.
Alisema Taasisi hiyo itatoa mtaalamu mshauri mmoja ambaye atafanya kazi
kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa muda wa
miaka mitatu ili kutoa ushauri na mapendekezo ya namna gani wata
kabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili jiji liwe salama.
No comments:
Post a Comment