Sunday, 2 July 2017

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ehud Olmert aachiliwa huru

Aliyekua waziri mkuu wa Israel Ehud Olmet, ameachiliwa huru baada kutumikia kifungo Gerezani kwa miezi kadhaa adhabu aliyopewa baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.
Makosa hayo na pia lile la kujaribu kuzuia mkono wa sheria kufanya kazi yake, anasemekana Aliyatenda alipokuwa waziri wa biashara nchini humo.
Olmert ni kiongozi wa kwanza aliyehudumu cheo cha uwaziri mkuu kufungwa jela huko Israel.
Alikua waziri mkuu toka mwaka 2006 hadi 2009.
Aliachiliwa huru kwa msamaha baada ya kutumikia theluthi mbili ya kifungo chake.
Pia kumekuwa na wasiwasi kuhusu kudhoofika kwake kiafya.

Mwezi uliopita wizara ya sheria nchini humo ilidokeza kuwa polisi walikua wakimchunguza Olmert kuhusiana na tetesi kuwa alifanikiwa kutoa kimagendo nyaraka alizoandika kwa minajili ya kuchapisha kitabu

No comments:

Post a Comment