Friday, 7 July 2017

Watumishi 6 wasimamishwa kazi Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi,amewasimamisha kazi kwa muda watumishi sita kutoka idara mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Lindi kutokana na kutoridhishwa na uwajibikaji wao kwenye halmashauri hiyo huku  akimwagiza Katibu Tawala wa mkoa huo Ramadhani Kaswa,kuunda tume ndogo mara moja kwa ajili ya kuwachunguza watumishi hao.
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi,ameyasema hayo katika  kikao cha baraza maalumu la madiwani la kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu taarifa za fedha za halmashauri ya wilaya ya Lindi kwa mwaka wa fedha  wa 2015-2016.
Kauli ya mkuu wa mkoa wa Lindi,kuwasimamisha  kazi kwa muda kwa watumishi sita halmashauri ya wilaya ya Lindi inaungwa mkono na madiwani wa halmashauri  hiyo.

Watumishi sita wa halmashauri ya wilaya ya Lindi waliosimamishwa kazi kwa muda kupisha uchunguni ni pamoja na afisa ushirika,mwanasheria,afisa ugavi,mhandishi,mweka hazina na mkaguzi wa ndani.

No comments:

Post a Comment